Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Mwinyi ateuwa watendaji wapya

Muktasari:

  • Miongoni mwa walioteuliwa ni Samora Chacha, anayekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Sera na Utafiti katika Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale.

Zanzibar. Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amefanya uteuzi wa watendaji sita katika taasisi tofauti akiwemo Samora Chacha, aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Sera na Utafiti katika Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale.

Kabla ya uteuzi huo, Chacha alikuwa mfanyakazi katika sekta binafsi.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo Ijumaa Januari 20, 2023 na kusainiwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Zena Said imesema, Adil Fauz George ameteuliwa kuwa mkurugenzi wa idara ya usimamizi na uratibu wa shughuli za utalii katika kamisheni ya utalii.

“Kabla ya uteuzi huo George alikuwa mfanyakazi wa sekta binafsi,” imesema taarifa hiyo.

Katibu mkuu mstaafu, Yakout Hassan Yakout ameteuliwa kuwa mjumbe wa kamisheni ya utumishi wa umma huku Ali Saleh Mwinyi ameteuliwa tena kwa kipindi cha pili kuwa mwenyekiti wa bodi ya shirika la magazeti.

Taarifa hiyo imesema Dk Mwinyi amemteua Safia Ali Rijaal ambaye ni mstaafu katika utumishi wa umma kuwa mwenyekiti bodi ya shirika la huduma za maktaba Zanzibar na Ussy Khamis Debe ameteuliwa kuwa katibu mtendaji wa baraza la taifa la watu wenye ulemavu

Uteuzi huo unaanza leo Januari 20, 2023