Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais amteua Kingai kuwa DCI

Muktasari:

  • Rais Samia Suluhu Hassan amempandisha cheo Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Ramadhan Kingai kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amempandisha cheo Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Ramadhan Kingai kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).

Kingai anachukua nafasi ya Camillus Wambura ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP).


Julai 15 mwaka huu, taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, David Misime ilisema kuwa Kingai amehamishwa kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma akitokea Mkoa wa Kinondoni.
 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumatano Julai 20, 2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus imeeleza kuwa Kingai anachukua nafasi ya Wambura ambaye ameteuliwa kuwa IGP.