Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

PPRA yaokoa Sh2.6 bilioni malipo hewa

Muktasari:

  • PPRA ilibaini hayo wakati wa utekelezaji wa majukumu yake katika ukaguzi wa taasisi 180 za Serikali, mashirika ya umma.
no

Dar es Salaam. Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) imeokoa zaidi ya Sh2.6 bilioni kwa kufanikiwa kuzuia malipo yaliyokiuka utekelezaji wa mkataba katika ununuzi wa umma pamoja na kusudio la baadhi ya wazabuni kukwepa kodi ya ongezeko la thamani (VAT). 

Hayo yalibainishwa leo Oktoba 7 na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi PPRA, Dk Leonada Mwagike alipokuwa akikabidhi ripoti ya ukaguzi katika ununuzi Serikalini kwa mwaka wa fedha 2022/2023 kwa Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande, hafla iliyofanyika jijini Dodoma hivi karibuni.

Dk Mwagike ameeleza kuwa PPRA ilibaini hayo wakati wa utekelezaji wa majukumu yake katika ukaguzi wa taasisi za Serikali, mashirika ya umma na wizara ambapo jumla ya Taasisi 180 zilikaguliwa. Ukaguzi huo ulijikita katika kuangalia taratibu za ununuzi na utekelezaji wa mikataba. 

Dk Mwagike amesema kutokana na ukaguzi uliofanyika, PPRA ilibaini baadhi ya wakandarasi walikwepa kulipa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) katika kazi walizozifanya Serikalini, hali hiyo ilipelekea PPRA kuelekeza wasilisho la stakabadhi hizo kabla ya l ukaguzi kwisha.

Jumla ya stakabadhi zenye thamani ya Sh290 milioni ziliwasilishwa.

 “Fedha zote hizi zilizopatikana kutokana na malipo ya kodi ya ongezeko la thamani zimerudishwa Serikalini," amesema mwenyekiti huyo.

meongeza kuwa fedha nyingine zilizookolewa  zilitokana na malipo yaliyolipwa kwa mtoa huduma ambayo hayakuwa sahihi, malipo hayo yenye thamani ya Sh233 milioni yalirejeshwa Serikalini. 

Vilevile, amesema malipo yenye thamani ya Sh1.7 bilioni yaliokolewa kutokana na kusitisha malipo ya  huduma iliyotolewa chini ya kiwango kwa moja ya Taasisi ya Umma, hali iliyofanya PPRA kuelekeza taasisi husika kukatisha mkataba na mzabuni.

 Dk Mwagike alieleza licha ya fedha hizo kurudishwa Serikalini kwa ajili ya matumizi mengine ya maendeleo, pia PPRA imemfungia mzabuni mmoja ambaye alihusika moja kwa moja na makosa ya kutoa huduma chini ya kiwango na kutaka kuisababishia Serikali hasara. Alisisitiza kwamba mzabuni huyo hataruhusiwa kutoa huduma yoyote Serikalini.

Katika ripoti hiyo, mamlaka ilipendekeza hatua mbalimbali kuchukuliwa na Serikali kwa Taasisi ambazo zimeisababishia Serikali hasara.

 “Mamlaka inatoa mapendekezo mbalimbali kwa Taasisi Nunuzi husika ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua za kinidhamu kwa watumishi waliohusika na mchakato wa ununuzi iliyosabaisha hasara kwa Serikali” Dkt. Mwagike

Hiyo ni ripoti ya 17 kuwasilishwa kutokana na tathmini ya mwaka ya utendaji kwa taasisi za umma ikiweka tamati ya ripoti zilizowasilishwa mbele ya Waziri wa Fedha ambapo kuanzia mwaka wa fedha 2023/24, ripoti hiyo rasmi itakuwa iikiwasilishwa moja kwa moja kwa Rais.

Akizungumzia hatua hiyo, mtaalamu wa uchumi, Oscar Mkude amesema PPRA wamefanya jambo kubwa lenye lengo la kusimamia matumizi ya Serikali kama ambavyo wamepewa mamlaka kisheria.

"Tanzania tuna Taasisi nyingi za Udhibiti lakini zimekuwa hazifanyi kazi zao kikamilifu, kwa hiyo walivjokifanya PPRA kiwe ni chachu kwa mamlaka nyingine za Serikali kutimiza wajibu wao wa kulinda rasilimali za umma katika maeneo yao," amesema Mkude.