Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

 PPRA yaibua madudu fedha za umma

Muktasari:

  • Ripoti ya Tathimini ya Utendaji ya mwaka wa fedha 2022/23, ambapo imebaini madudu katika taasisi mbalimbali za umma.

Dodoma. Uchunguzi na ukaguzi maalumu uliofanywa na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) kwa taasisi 12 umeonyesha kuwa Serikali ilipata hasara ya Sh8.77 bilioni kutokana na ukosefu wa uwajibikaji ufanisi, uwazi na uadilifu.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya PPRA, Dk Leonada Mwagike ameyasema hayo leo Ijumaa Septemba 29, 2023 wakati akikabidhi Ripoti ya Tathimini ya Utendaji ya mwaka wa fedha 2022/23 kwa Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Chande.

Dk Leonada amesema kati ya taasisi 180 zilizokaguliwa na PPRA, 28 zilikuwa na matokeo ya kuridhisha, 109 zilikuwa na matokeo ya wastani na 43 zilikuwa na matokeo hafifu.

Amesema kati ya taasisi 43 zilizopata matokeo hafifu, 28 zilikuwa kwenye kundi la tawala za mikoa na Serikali za mitaa, nane ni mashirika ya umma huku saba zikiwa ni wizara, idara za Serikali zinazojitegemea na wakala wa Serikali.

“Katika mwaka wa fedha 2022/23 mamlaka ilifanya uchunguzi na ukaguzi maalum kwa taasisi 12 na matokeo yanaonyesha kuwa Serikali ilipata hasara ya Sh8.77 bilioni kutokana na ukosefu wa uwajibikaji ufanisi, uwazi na uadilifu kwenye taasisi zilizokaguliwa na kuchunguzwa,”amesema.

Amesema Serikali iliokoa fedha zenye thamani ya Sh2.26 bilioni ilitokana na kurejeshwa kwa malipo ya awali, Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na kuzuiwa kwa malipo yaliyokiuka utekelezaji wa mikataba.

Dk Leonada amesema matokeo ya ukaguzi na uchunguzi maalum ni pamoja na kuokoa kutoa zabuni zenye thamani ya Sh485 bilioni kwa wazabuni wasio na sifa, tathimini isiyo ya haki ya zabuni zenye thamani ya Sh366.07 bilioni.

Mengine ni kutokuwepo kwa ushindani katika ununuzi wa umma wenye thamani ya Sh209.98 bilioni na ununuzi wa bidhaa zenye thamani ya Sh5.07 bilioni bila kuomba stakabadhi za Kieletroniki (EFD).

Ametaja matokeo mengine ni ununuzi wa bidhaa wenye thamani ya Sh661.68 bilioni kwa stakabadhi za kughushi na usimamizi mbovu wa mikataba ya ujenzi yenye thamani ya Sh8.8 bilioni uliosababishwa na kuchelewa na kutokamilika kwa miradi.

Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Chande ameziagiza taasisi nunuzi zote kuhakikisha zinafanya ununuzi wa umma kupitia mfumo wa NeST kuanzia Oktoba Mosi mwaka 2023. 


“Naagiza hatua kali zichukuliwe kwa wote watakaokiuka maelekezo haya. Katibu Mkuu Hazina na Mlipaji Mkuu wa Serikali na kuelekeza kuwa hili ulisimamie na kulifuatilia kwa karibu mnoooo,” amesema.

Amesema Serikali imepata hasara ya jumla ya Sh8.77 bilioni kutokana na ukosefu wa uwajibikaji, ufanisi, uwazi, na uadilifu kwenye taasisi 12 zilizochunguzwa.

Amesema vitendo hivyo vya jinai vinavyohujumu uchumi wa nchi na hivyo hatua kali hazina budi kuchukuliwa kwa wahusika wote.