Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Polisi yadhibiti maandamano Dar

Muktasari:

Kutokana na kuwepo kwa taarifa za maandamano, Jeshi la Polisi limeimarisha ulinzi maeneo mbalimbali katikati ya Jiji la Dar es Salaam, huku baadhi ya watu waliojitokeza wakionekana katika maeneo hayo.


Dar es Salaam. Kutokana na kuwepo kwa taarifa za maandamano, Jeshi la Polisi limeimarisha ulinzi maeneo mbalimbali katikati ya Jiji la Dar es Salaam, huku baadhi ya watu waliojitokeza wakionekana katika maeneo hayo.

Juni 15 mwaka huu mwanachama wa Chadema, Deus Soka ambaye aligombea udiwani kupitia chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa 2020, alitangaza kuitisha maandamano kupinga mkataba wa ushirikiano wa uendeshaji wa bandari kati ya Kampuni ya DP World na Serikali ya Tanzania.

Hata hivyo Juni 17, 2023 Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam lilipiga marufuku maandamano hayo na kueleza kuwa, mtu aliyeandaa ameshajibiwa kwa barua.

 Deus Soka

Maandamano hayo yalipangwa kuanzia Temeke kwenda Ikulu ya Magogoni kupitia maeneo mbalimbali ikiwemo Keko, Karume, Kariakoo na Mnazi Mmoja lakini leo walibadilisha na kutangaza kuanzia Mnazi Mmoja.

Mwananchi Digital limezunguka maeneo mbalimbali na kukuta baadhi watu wakiwa wametawanyika maeneo mbalimbali, huku gari za polisi zikizunguka maeneo hayo.

Mmoja wa wafuasi katika maandamano hayo, Shabani Kirita amesema bado wanakusudia kufanya maandamano kwa kuwa ni ya amani na hawafanyi fujo yoyote.

 "Tunaendelea kukusanyika lazima tuyafanye licha ya polisi kupiga marufuku, maandamano ni haki yetu kikatiba Polisi wanachotakiwa ni kutulinda,"amesema Kirita.

Juni 10, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha azimio kuhusu pendekezo la kuridhiwa kwa mkataba baina ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai kwa lengo la kuanzisha ushirikiano katika uendelezaji wa maeneo ya bandari nchini.

Pendekezo hilo liliwasilishwa bungeni Juni 10, na kupitishwa na Bunge baada ya wabunge kupata fursa ya kuchangia na kuishauri Serikali kuhusu mkataba huo.