Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

No Reform No Election, Oktoba Tunatiki yatajwa kuchochea fujo Oktoba 29

Matairi yakiwa yanawaka moto baada ya kuchomwa katika moja ya mitaa ya Jiji la Dar es Salaam wakati wa ghasia za Oktoba 29, 2025. Picha na Mtandao

Dar es Salaam. Tume ya Kuchunguza Matukio ya Oktoba 29 imesema baadhi ya kaulimbiu za kisiasa kama vile ‘Otoba tunatiki’, ‘No Reform no Election’, ‘Oktoba Tunatoka’ na ‘Tumedhamiria uchaguzi’ ni miongoni mwa kauli zilizochochea vurugu.

Kauli zingine za kisiasa zilizochochea vurugu hizo ni Samia Must go, Tunataka kukomboa nchi yetu, hakuna uchaguzi ndani ya Serikali hii na tunahakikisha nchi haisimami hadi mpaka Serikali iondoke.

Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mkuu Mstaafu, Othman Chande wakati akiwasilishwa ripoti yao ikiwamo kutaja vichocheo vitatu vilivyohamasisha ghasia wakati na baada ya uchaguzi mkuu.

Vichocheo hivyo ni mitandao ya kijamii ambapo kwa mujibu wa mashuhuda.

Chande amesema mitandao yao ilitumika kabla na wakati wa uchaguzi mkuu kwa kiwango kikubwa kuliko ilivyowahi kutokea nchini.

Amesema wahusika walibuni mada kwenye mitandoa ya kijamii ikiwemo mada ya kuhamasisha wananchi kutoshiriki uchaguzi huo au kuhakikisha haufanyiki.

Chande amesema mitandao hiyo imetumika pia kuandaa mada ya majadiliano na kupanga mbinu na kuwaelekeza waliokubali kushiriki vurugu katika uchaguzi namna ya kufanikisha lengo hilo.

Amesema wapo pia mashahidi walioshiriki ghasia walikwenda mbele ya Tume na kukiri kwamba baadhi yao walipewa simu maalumu za mikononi na kupewa kazi ya kupiga picha na video ya majeruhi na vifo au kupiga picha jirani na magari ya jeshi na maeneo yenye ghasia na video hizo wazitume kwenye mitandao ili kupandisha hasira ya watu, ili nao washiriki maandamano hayo na waliaminishwa Jeshi la Polisi lipo upande wao.

Chande amesema kundi la pili la vichocheo, ambavyo ni kauli za baadhi ya wanasiasa zilizogeuka kuwa kaulimbiu za waliofanya ghasia, ikiwamo hakutakuwa na uchaguzi bila mabadiliko ya mfumo, Serikali imepoteza uhalali wa kuongoza nchi, lazima shinikizo la wananchi liongoze hadi Serikali iondoke, mchakato wa kupata wagombea umekiuka taratibu, wagombea siyo halali na mchakato urudiwe.

Kundi la tatu la vichocheo lilihusu baadhi ya maeneo ya nchi ambao wagombea wa viti vya udiwani na ubunge majina yao yalikatwa kwenye ngazi za juu za vyama na hivyo kuona ghasia zilizokuwa zinafanywa zitawasaidia kupata mabadiliko ya mfumo wa ndani ya vyama vyao na wao kuhamasisha wafuasi wao chini chini kushiriki fujo hizo.