Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

NEMC yatoa elimu ya mazingira kwa wadau 1,450 Nanenane

Muktasari:

  • NEMC imewafikia wadau 1,450 katika kuwapa elimu ya uhifadhi na usimamizi wa mazingira katika maonesho ya kilimo ya Nanenane yaliyofanyika Dodoma, yapongezwa na wadau elimu ya mazingira maonesho ya nanenane

Dodoma. Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limewafikia wadau takriban 1,450 katika kutoa elimu ya uhifadhi na usimamizi endelevu wa mazingira kwenye Maonesho ya Kilimo ya Nane Nane jijini Dodoma na viwanja vya John Mwakangale, Mbeya.

Elimu hiyo ilijikita kwenye mbinu bora za kilimo hifadhi, ufugaji endelevu, uvuvi salama na ulinzi wa vyanzo vya maji, sambamba na umuhimu wa kufanya tathmini ya athari kwa mazingira kabla ya kuanzisha miradi ya maendeleo, hasa ya kilimo.

Ofisa Mazingira wa NEMC, Dalia Kilamlya, amesema elimu hiyo inalenga kuwajengea uwezo wananchi na wawekezaji kufanya maamuzi sahihi yanayozingatia mustakabali wa mazingira.

“Tunawahimiza wawekezaji kusajili miradi yao na kupata vyeti vya mazingira kama kigezo cha kuendesha shughuli kisheria na kwa kuzingatia hifadhi ya mazingira,” amesema.

Kwa mujibu wa NEMC, hatua hiyo ni sehemu ya jitihada za kuelimisha makundi mbalimbali nchini kuhusu athari za uharibifu wa mazingira ikiwamo uchomaji moto hovyo, ukataji miti na utupaji taka, ambazo zinachangia mabadiliko ya tabianchi, mmomonyoko wa ardhi na upungufu wa rasilimali maji.

Meneja Mawasiliano wa NEMC, Irene John, amesema mwitikio wa wadau umekuwa mkubwa, jambo linalotoa matumaini ya mabadiliko chanya. 

“Mazingira lazima yatunzwe ili yatutunze, ndiyo maana mkazo wetu tunahitaji watanzania waelewe umuhimu wa hifadhi wa mazingira ili wayaliende kutokana na manufaa yake,” amesema