NEMC kubadilisha historia shule ya msingi Arusha

Mkurugenzi wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira na Jamii kutoka NEMC, Lilian Lukambuzi akizungumza baada ya kukabidhi majiko hayo
Muktasari:
- NEMC yatoa majiko manne yanayotumia nishati safi ya kupikia kwa shule ya msingi Arusha yenye uwezo wa kupika chakula chenye ujazo wa lita 700 kwa wakati mmoja, na yatasaidia wanafunzi zaidi ya 1,6000.
Dar es Salaam.

Majiko hayo yamekabidhiwa katika shule ya Msingi ya Arusha inayotoa huduma ya chakula kwa wanafunzi takribani 1, 600, ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikitumia nishati
ya kuni na mkaa kwa asilimia 100 katika kupika chakula.
Akizungumza kwaniaba ya mkurugenzi mkuu wa NEMC,Dk Immaculate Semesi, katika hafla ya kukabidhi majiko hayo, Mkurugenzi wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira na Jamii kutoka taasisi hiyo, Lilian Lukambuzi amesema kuelekea kilele cha siku wa wanawake duniani, Baraza linaenda kubadilisha historia ya shule hiyo.
"Shule hii imekuwa ikitumia nishati
ya kuni na mkaa kwa asilimia 100 katika kupika chakula. Kwa
niaba ya Mkurugenzi Mkuu Dk Immaculate Sware Semesi Baraza
linakabidhi majiko manne (4) ya nishati safi ya kupikia (gas stoves)
yenye uwezo wa kupika chakula chenye ujazo wa lita 700 kwa
wakati mmoja," amesema

Akitoa mchangamuo wake Lilian amesema katika majiko hayo, majiko matatu (3) yana ujazo wa lita 200 kila moja gharama yake ni 2.4milioni kwa kila moja na jiko moja lina ujazo wa lita 100 lenye gharama ya Sh 1.6 milioni
Kulingana na maelezo ya Lilian amesema gharama ya jumla kwa majiko na gesi ni takribani sh 10 Milioni, huku akieleza wanaunga mkono juhudi za Rais Samia akiwa ni kinara wa matumizi ya nishati safi ya kupikia barani Afrika.
"Pia juhudi hizi ni kutekeleza mkakati wa Taifa wa matumizi ya nishati safi ya kupikia uliozinduliwa mwaka jana 2024 unaolenga kuhakikisha kuwa ifikapo 2034 asilimia 80 ya watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia ili kulinda mazingira, afya ya jamii na kuboresha maisha.," amesema.
Lilian amesema kutoa majiko hayo ni katika kuunga mkono utekelezaji wa maelekezo ya serikali kuhusu taasisi zinazolisha watu zaidi ya 100 kuachana na matumizi ya kuni namkaa na kuhamia kwenye matumizi ya nishati safi ya kupikia.
"Matumizi ya mkaa na kuni (nishati chafu) yanayochangia uharibifu
wa mazingira kutokana na ukataji miti, kuathiri afya ya jamii
kutokana na moshi hasa kwa wanawake na watoto ambao
hutumia muda mwingi jikoni," amesema nakuongeza
"Majiko haya tunayokabidi katika shule ya Msingi Arusha tunaamini
yatasaidia wapishi kukamilisha majukumu yao kwa ufanisi zaidi na
kwa wakati. Hivyo pia itasaidia kuboresha afya na ustawi wa
wanafunzi na taifa kwa ujumla," amesema
Amesema wanapoelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake
duniani wanaendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya
kupikia kwani huongeza ufanisi kwa kuokoa muda wa kupika na
kutoa muda kwa wanawake kushiriki katika shughuli
nyingine za kiuchumi