Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

NCCR- Mageuzi ‘yaibipu’ polisi

Katibu Mkuu wa  Chama cha NCCR-Mageuzi Juju Danda

Muktasari:

Danda ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi) wakati akizungumza na wanahabari juu ya hali ya kisiasa nchini.

Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa  Chama cha NCCR-Mageuzi Juju Danda amesema chama hicho kinakusudia kufanya mikutano ya hadhara katika maeneo mbalimbali ya nchi ili kujiimarisha na kupata wanachama wapya.

Danda ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi) wakati akizungumza na wanahabari juu ya hali ya kisiasa nchini.

Amesema  kifungu namba 11 cha Sheria ya Vyama vya Siasa kinavipa haki vyama vyenye usajili wa  muda na wa kudumu kufanya mikutano ya hadhara na maandamano kwa ajili ya kujitangaza na kutafuta wanachama wapya.

"Hizi ni salama tu kwa watawala.Muda ukifika tutangaza lini tunaanza, wapi tutaanzia na kuishia ili kukiimarisha chama.

"Mikutano ya ndani ya tumeshaifanya sana, sasa ni wakati wa mikutano ya hadhara ili kuubarisha umma kinachoendelea," anasema Danda.

Hata hivyo mpango huo wa chama hicho hautofanikiwa kutokana na polisi kwa nyakati tofauti kutangaza kupiga marufuku mikutano ya hadhara na maandamano.