Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mume, mke wauawa kwa upanga Moshi

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa

Muktasari:

Mume na mke wauwawa kwa kukatwakatwa na panga kwa madai wamekuwa wakimroga mtoto wa ndugu yao.

Moshi. Jeshi la polisi Mkoani Kilimanjaro linamshikilia Jonas Mushi (26) mkazi wa kijiji cha Manushi kati Wilaya Moshi, kwa tuhuma za kwa kuwauwa  kwa kuwakata panga watu wawili  ambao ni mke na mume kutokana na imani za kishirikina.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kwamba yalitokea  Julai 19 , 2022 majira ya saa 17:45 jioni, ambapo amesema  mtuhumiwa aliwakatakata kwa panga Paul Mushi (70), Felista Mariki Mushi (65), ambao ni mke na mume hadi kupoteza maisha kwa madai kuwa wamekuwa wakimloga.

Kamanda amesema mtuhumiwa alifika kijijini hapo jana akitokea Kibaha mkoani Pwani na alipofika nyumbani alichukua panga na kuelekea nyumbani kwa baba yake mkubwa ambae ni marehemu.

“Mtuhumiwa alipofika nyumbani kwa marehemu, alianza kumshambulia kwa kumkatakata sehemu mbalimbali za mweli hadi kupoteza maisha.

 “Wakati akifanya kitendo hicho mke wake ambae ni marehemu alimkuta mtuhumiwa akimshambulia mume wake na kujaribu kumsaidia ndipo mtuhumiwa alipoanza kumshambulia na kumkatakata kwa panga hadi kupoteza uhai," amesema.

Kamanda amewataka wananchi kuacha imania potofu za kishirikina na kwamba serikali haitasita kumchukulia hatua mtu yeyote atakaye jichukulia sheria mkononi.