Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mume aliyeua mke kisa njaa afungwa kifungo cha nje

Muktasari:

  • Mke aliachiwa Sh6,000 za kupika chakula, akaondoka kwenda kulewa, akarudi usiku wa manane.

Sumbawanga. Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga, imemhukumu David Godfrey kutumikia kifungo cha nje cha miezi 12 baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumuua mkewe, Hawa Selemani, bila kukusudia kutenda kosa hilo.

Katika hukumu aliyoitoa Aprili 24, 2025, Jaji Thadeo Mwenempazi amesema Hawa (marehemu) ndiye kiini cha mauaji kwa kutomjali mume wake aliyekuwa na njaa, badala yake akaenda kwenye ulevi wa pombe na marafiki hadi usiku wa manane.

Tukio la mauaji lilitokea Oktoba 7, 2024. Mshtakiwa, aliyekuwa akifanya kazi za vibarua za kubeba takataka, alipofanya kazi hiyo Oktoba 6 mwaka huo na kulipwa ujira wa Sh6,000, alizompelekea mkewe nyumbani ili aandae chakula kwa ajili yao.

Baada ya kumkabidhi mkewe fedha, mchana aliondoka na kwenda kuwatembelea marafiki zake na kurudi saa 1:00 usiku na hakukuta chakula na mkewe hakuwapo.

Aliondoka na kurudi saa 3:00 usiku alipokuta hali ikiwa vivyo hivyo.

Mshtakiwa aliamua kulala hadi ilipofika saa 6:00 usiku ndipo mkewe alirudi akiwa mlevi wa kupindukia, akiwa amesindikizwa na mwanamume aliyetimua mbio baada ya kumuona mshtakiwa, huku nyuma akiacha tafrani baina ya wawili hao.

Kitendo cha mkewe kilimuudhi mshtakiwa na kumsababisha kumpiga mkewe kwa kutumia fimbo hivyo akapata jeraha kichwani. Kwa kuwa alitumia fimbo, alisababisha atokwe damu.

Mshtakiwa alitumia kipande cha nguo kuzuia damu isiendelee kutoka, wakaenda kulala. Asubuhi aliondoka kwenda kutafuta vibarua, lakini akakamatwa na Polisi saa 2:00 asubuhi, mkewe akifariki dunia dakika 45 baadaye.

Jaji amesema ni suala lililopo katika mwenendo wa kesi hiyo kuwa mshtakiwa ana mtoto mdogo mwenye umri wa miaka minne na kwamba, hakuna ubishi alichokozwa na mkewe (marehemu) na kutenda kosa hilo la kwanza kwake.

“Mshtakiwa alikiri kutenda kosa hilo. Nachukulia hii kama ishara kuwa anajuta kwa yale aliyomfanyia mkewe. Ingawa mwendesha mashtaka ameomba nitoe hukumu kali, mimi huwa nakubaliana na utetezi apewe adhabu nafuu.

“Kwa maoni yangu, kwa mazingira ya tukio lenyewe yangeweza kuathiri mawazo na tahadhari yake kwa yale aliyofanya. Anajituma sana kikazi, lakini mkewe alikuwa hajali kiasi cha kutomhudumia mumewe mwenye njaa,” amesema Jaji.

Amesema mkewe (marehemu) alienda kunywa pombe na marafiki zake na kurudi usiku wa manane, na kutokana na sababu hiyo ameona amhukumu kifungo cha nje cha miezi 12 na katika kipindi hicho hapaswi kutenda kosa la jinai.