Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Baba jela miaka 30 kwa kumpa ujauzito binti yake

Baba mbaroni akidaiwa kubaka wanawe

Muktasari:

  • Mshtakiwa Daud Mabele alidaiwa kutenda kosa mkewe alipokuwa amekwenda nyumbani kwao kujifungua.

Simiyu. Daud Mabele (38), mkazi wa Kijiji cha Kakola, Kata ya Shishiyu wilayani Maswa, mkoani Simiyu amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kumuingilia kimwili na kumpa ujauzito binti yake wa kumzaa.

Mabele pia ameamriwa kumlipa binti yake (14) fidia ya Sh200,000.

Hukumu imetolewa jana Alhamisi Aprili 24, 2025 katika Mahakama ya Wilaya ya Maswa na Hakimu Mkazi, Aziz Khamis baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka.

Mshtakiwa alishtakiwa kwa kosa la kumwingilia kimwili mwanaye wa kumzaa (maharimu) kinyume cha kifungu cha 158(1) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2022.

Katika kesi hiyo ya jinai namba 6929/2025, Kwa mujibu wa hati ya mashtaka na ushahidi uliowasilishwa mahakamani, mshtakiwa alitenda kosa hilo usiku wa tarehe isiyofahamika Septemba, 2024.

Alidaiwa kutenda kosa hilo nyumbani kwake baada ya mama wa binti huyo, ambaye ni mke wake kwenda nyumbani kwao kujifungua. 

Katika kuthibitisha mashtaka, upande wa Jamhuri uliwaita mahakamani mashahidi watano akiwamo mwathirika (binti aliyetendewa kitendo hicho) na uliwasilisha kielelezo kimoja.

Akijitetea mshtakiwa alikana shtaka akidai hakuna ushahidi wa moja kwa moja unaoonyesha alitenda kosa hilo.

Pia alihoji uhalali wa ushahidi wa mlalamikaji kutokana na mazingira ya kifamilia yaliyokuwa na migogoro kabla ya tukio hilo kudaiwa kutokea, akidai inawezekana kuna nia ya kumchafua.

Baada ya mshtakiwa kutiwa hatiani upande wa mashtaka uliomba mshtakiwa apewe adhabu kali ili iwe fundisho kwake na onyo kwa wengine wenye nia au lengo la kufanya kitendo kama hicho.

Kesi hiyo iliendeshwa na mwendesha mashtaka wa Jeshi la Polisi, Vedastus Wajanga.

Mahakama baada ya kusikiliza ushahidi wa upande wa mashtaka na wa utetezi iliridhika kuwa upande wa mashtaka ulithibitisha shtaka dhidi ya amshtakiwa kama alivyoshtakiwa, hivyo ikamtia hatiani kwa kosa hilo.

Baada ya kumtia hatiani, kabla ya kumsomea adhabu, hakimu alitoa nafasi kwa upande wa mashtaka kueleza historia ya uhalifu wa mshtakiwa, huku akimpa mshtakiwa fursa ya kuomba shufaa (nafuu ya adhabu).

Mwendesha mashtaka, Wajanga aliieleza mahakama kuwa hawana kumbukumbu za nyuma za mshtakiwa.

Hata hivyo, aliiomba Mahakama itoe adhabu kali ili iwe fundisho kwake na onyo kwa wengine wenye nia au lengo la kufanya kitendo alichofanya mshtakiwa.

Mshtakiwa aliiomba mahakama impunguzie adhabu akidai ni mkosaji wa mara ya kwanza na ana familia inayomtegemea.

“Ukizingatia kuwa kitendo alichokifanya mshtakiwa ni kinyume cha sheria na maadili ya Mtanzania na kitendo hicho kimeacha alama ambayo haitafutika kwa muathirika, na kwa kuzingatia kuwa muathirika ameachiwa ujauzito wa miezi saba na ni ukatili wa kijinsia ni vizuri apatiwe hukumu kali,” amesema hakimu na kutamka adhabu:

"Kwa hiyo mahakama hii baada ya kumtia hatiani mshtakiwa Daudi Mabele, kama alivyoshtakiwa, basi sasa Mahakama hii inamuadhibu mshtakiwa kutumikia kifungo cha miaka 30 jela. Pia mshtakiwa anaamriwa kumlipa muathirika fidia ya Sh200,000.”