Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Muhimbili yawapokea wanafunzi Wasudan 150, kuendelea na mafunzo

Wanafunzi wa udaktari Chuo Kikuu cha Tiba, Sayansi na Teknolojia (UMST) cha Khartoum nchini Sudan 

Muktasari:

  • Kutokana na machafuko yanayoendelea katika mji wa Khatom nchini Sudan, jumla ya wanafunzi 650 wanaotarajiwa kumalizia mwaka wao wa mwisho wa udaktari unaohusisha mafunzo kwa vitendo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Dar es Salaam. Wanafunzi 150 kutoka Chuo Kikuu cha Afya, Sayansi na Teknolojia (UMST) wamewasili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa ajili ya kumalizia mwaka wa tano wa masomo yao unaohusisha mafunzo kwa vitendo.

Wanafunzi hao ni miongoni mwa 650 wanaotarajiwa kuhitimisha shahada zao za udaktari Muhimbili watakaokuja kwa awamu kufuatia machafuko yanayoendelea nchini Sudan.

Zaidi ya watu 400 wamekufa na maelfu wamekimbia maafa kutokana na vita ya wenyewe kwa wenyewe inayoendelea Sudan, ambayo ililipuka kuanzia Aprili 15, 2023.

Akizungumza leo Juni 19, 2023 wakati akiwatambulisha wanafunzi hao, Mkurugenzi wa Muhimbili, Profesa Mohamed Janabi amesema wanafunzi hao kwa kipindi kirefu wameshindwa kuendelea na masomo yao tangu vita hivyo vianze.

Amesema kwa kuwa Muhimbili ni hospitali kubwa kwani inaona wagonjwa 2,700 kwa siku na kulaza 1,500 wanafunzi hao wanaweza kujifunza vizuri zaidi kwani pia ina wataalamu wa kutosha.

"Sudan kuna machafuko badala ya kukaa nyumbani hawa vijana tumewapokea watakuwa na sisi kwa mwaka mzima kumaliza masomo yao au mpaka kutakapotulia.

"Hili ni kundi la kwanza. Hakuna upungufu wa walimu, tumejipanga vizuri watakuja wengine 500, Hawa wameshakuwa na sisi karibu wiki nzima sasa na watajifunza na kufanya mitihani," amesema Profesa Janabi.

Mmoja kati ya wanafunzi hao, Ruba Anwar Salih amesema wamefurahi kupata nafasi hiyo kwakuwa walitamani kumaliza masomo yao nchi yenye amani.

"Tanzania ina amani na tunashukuru kwa kuwa Muhas ni chuo kinachofanya vizuri kitaaluma hivyo Muhimbili ni hospitali bora kwa mafunzo," amesema Ruba.

Mwanzilishi na Makamu Mkuu wa Chuo cha UMST,  Profesa  Mamoun Homeida ameishukuru Tanzania kwa kutoa nafasi ya kuwapokea wanafunzi hao kwa ajili ya kumalizia mwaka wao wa mwisho.