Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtoto auawa na mamba akifua nguo mtoni Masasi

Muktasari:

  • Mtoto huyo aliyekuwa akifua nguo na wenzake kando ya mto Ruvuma alirukiwa na mamba na kuvutwa ndani ya maji, lakini baadaye mwili wake uliopolewa akiwa ameshafariki.

Mtwara. Mtoto Ramla Said (13) amefariki baada ya kushambuliwa na mamba alipokuwa akifua nguo na wenzake pembeni ya mto Ruvuma katika Kijiji cha Lichehe kata ya Sindano Wilayani Masasi.

Akingumza kwa simu na Mwananchi leo Julai 27, baba wa mtoto huyo, Saidi Chalido amesema tukio hilo lilitokea Julai 22 wakati mtoto huyo alikuwa ni mwanafunzi wa darasa la saba shule ya msingi Mgwagule.

“Huyu mtoto alitoka hapa akiwa na wenzie wakaaga kuwa wanakwenda mtoni kufua, lakini ilipofika majira ya saa nne asubuhi nilipata taarifa ya mwenzao amevutwa na mamba mtoni,” amesema Chalido.

Akizungumzia tukio hilo, Diwani wa kata ya Sindano Rashid Masudi Mchelelo amesema kabla ya kwenda mtoni, mtoto huyo alimfuata baba yake na kumuomba pesa ya kununua sabuni ya kufulia ikiwa ni majira ya saa 1 asubuhi.

“Baada ya kupewa Sh1, 000 alikwenda dukani na kurejea na sabuni ya kipande na ya unga kisha akaelekea mtoni akiwa na wenzake wawili,” amesema.

Amesema watoto waliokwenda kufua naye wamesema kuwa akiwa ameinama anaendelea kufua ghafla waliona mamba akimrukia mwenzao na kumjeruhi ambapo alimvuta na kumzamisha kwenye maji huku wenzake wakishindwa kumsaidia.

“Walipiga kelele na mayowe ya kuomba msaada na ndipo kijana aliyekuwa karibu na eneo hilo alifika na msaada wa kumuokoa mtoto huyo, japo alikuwa tayari amefariki,” amesema Mchelelo.