Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtanzania mcheza Judo atunukiwa tuzo Japan

New Content Item (2)

Mtanzania Dudley Mawalla (kushoto) akipokea cheti kutoka Balozi wa Japan hapa nchini Yasushi Misawa ikiwa ni katika kutambua mchango wake katika kueneza utamaduni wa Japan hapa nchini.

Muktasari:

  • Japan kupitia Wizara yake ya Mambo ya Nje imemtunuku Mtanzania, Dudley Mawalla tuzo ya heshima katika hatua ya kutambua mchango wake wa kukuza uhusiano kati ya nchi hiyo na Tanzania kupitia michezo ya Judo na Karate.

Dar es Salaam. Japan kupitia Wizara yake ya mambo ya nje imemtunuku Mtanzania, Dudley Mawalla tuzo ya heshima katika hatua ya kutambua mchango wake wa kukuza uhusiano kati ya nchi hiyo na Tanzania.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi tuzo leo jijini hapa balozi wa Japan hapa nchini, Yasushi Miwasa amesema wameamua kumtunuku Mawalla tuzo ya heshima kwa kutambua mchango wake kwa kuendeleza utamaduni wa Kijapani, ikiwemo Michezo ya Judo na Karate hapa nchini.

"Juhudi za Mawalla hadi sasa katika kueneza utamaduni wa Kijapani nchini Tanzania ni kubwa kwelikweli. Nikiwa Balozi wa Japan nchini Tanzania, ninayefanya kazi ya kukuza uhusiano wa Japan na Tanzania, napenda kutoa shukrani zangu za dhati na pongezi kwa Mawalla,” amesema Balozi Misawa.

Kwa upande wake Dudley Mawalla amesema anajisikia vizuri na anashukuru kwa kutambuliwa ingawa ni jambo la kushangaza kwake, kwa sababu amekuwa akifanya Judo kwa miaka 15 nyuma.

"Mimi naita Judo ni mtindo wa maisha, ukiitazama unafikiri ni mchezo tu lakini kuna mambo mengi kwenye judo," ameeleza.

Pia ameeleza jinsi Judo ilivyomnufaisha ambapo alisema ilimsaidia katika mambo yake ya kazi, jinsi ya kushughulikia mtazamo wake na jinsi ya kuwasiliana na watu mbalimbali anaokutana nao.

Mawalla pia amewataka wazazi kuwaruhusu watoto wao kujifunza mengi kuhusu Judo kwa sababu ni njia ya maisha.

Mawalla ni mbunifu kitaaluma na mkurugenzi mkuu wa MD Consultancy Limited, bila kusahau taaluma yake katika Judo, anatambulika kama Mkufunzi wa 2 wa DAN Black Belt.

Naye Rais wa Chama cha Judo hapa nchini (JATA) Zaidi Hamisi amesema kwa upande wake anaweza kumtambua kuwa ni mwanzilishi wa Judo nchini kutokana na ukweli kwamba amefanya mambo mengi kuhakikisha aina hiyo ya mchezo inafahamika ndani ya nchi.

"Kama mmoja wa wanafunzi wake naweza kusema yeye ndiye mwanzilishi wa judo katika nchi yetu, kwa sababu amefanya mambo mengi kama kuanzisha chama," amesema Zaidi.

Pia amesema wanajipanga kuanzisha programu ya Judo mashuleni kwa lengo la kutoa elimu kuhusu mchezo wa Judo kwani ni mchezo ambao umekuwa ukikua kwa kasi katika miaka ya hivi karibuni.

"Judo ni mchezo ambao kwa sasa unakua kwa kasi, kama chama tunataka kuanza na watoto kwa sababu ni wazuri kutokana na akili zao kuwa na uwezo katika kunasa vitu mbalimbali, ndiyo maana tunataka kuanzisha programu ya aina hii," amesema.

Aidha amesema kuwa tayari wameshapeleka mapendekezo Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na mambo yakienda sawa wataanza na shule chache katika mikoa tofauti ikiwemo Dar es Salaam, Dodoma, Morogoro, Arusha na Kigoma.