Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mradi wa maji Sh83 bilioni kunufaisha wakazi Pwani

Muktasari:

  • Mradi huo uliogharimu zaidi ya Sh83 bilioni umetekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) umehusisha upanuzi wa uwezo wa mtambo kutoka uzalishaji wa lita milioni 7.2 hadi lita milioni 21.6 kwa siku.

Pwani. Kaya 43,311 zenye idadi ya watu 303,180 mkoani Pwani wanatarajia kunufaika na na mradi wa maji uliotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (Dawasa).

 Mradi huo wa maji uliopo katika kituo cha daraja la Wami umehusisha upanuzi wa mtambo wa kuzalisha maji uliopo katika mto huo.

Zaidi ya Sh83 bilioni zimetumika hadi kukamilika kwake ambapo mtambo umepanuliwa kutoka uzalishaji wa lita milioni 7.2 hadi lita milioni 21.6 kwa siku.

Akizungumza wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge Uwekezaji na Mitaji ya Umma, Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa, Kiula Kingu amesema mradi umehusisha ujenzi wa matenki 18 ya kuhifadhi maji pamoja na ujenzi wa vioski vya kuchotea maji ambavyo tayari vimekamilika.

Amesema kupitia vioski 842 wateja wao ambao ni zaidi ya 7300 watapata maji ya uhakika mkoani humo.

Akizungumza mwenyekiti wa kamati hiyo (PIC) Deo Sangu, amesema hatua hiyo ni muhimu kwa mamlaka kwani wanaonufaika ni wananchi wa mkoa huo.

Sangu amesema kamati wameielekeza Serikali, kuhusu madeni ambayo Dawasa inaidai taasisi za kiserikali kiasi cha Sh13 bilioni ili iiongezee nguvu mamlaka hiyo kuendelea kutoa huduma kwa watu.

"Madeni ya maji ya taasisi yaweze kulipwa ili kazi ya kusambaza maji kwa wananchi kupitia miradi kama huu wa Chalinze awamu ya tatu iweze kuleta tija kwa wananchi,” amesema.

Aidha ameipongeza Menejimenti ya Dawasa kwa jitihada wanazofanya za kuhakikisha huduma ya maji inawafikia wananchi wote.

Kwa upande wake, Mbunge wa jimbo hilo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete amesema wakati anafanya mikutano jimboni humo wananchi walikuwa wakimletea chupa zenye maji meusi yenye tope wakiwa na maana wana shida ya maji.

Amesema anaishukuru Serikali kwa kutenga pesa zilizotekeleza awamu za miradi ambapo kwa sasa wananchi wanapata maji.

Akizungumzia changamoto Ridhiwani amesema bado wananchi wanatembea umbali mrefu kuvifuata vioski vya maji.

“Kioski kinaweza kuwa upande wa pili wa daraja, (daraja la Wami) hivyo mtu anapaswa kutembea kufuata maji. Tunajua malengo ya mradi ni wananchi wafikishiwe maji majumbani.

“Rais anataka kuona mama anatuliwa maji kichwani akasema Dawasa itenge kiasi cha Sh500 milioni kuhakikisha maji yanafika maeneo yote,” amesema Ridhiwani.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge amesema kwa upande wa kuweka mazingira bora ya uwekezaji mkoani humo maji ni kiungo muhimu ambapo wananchi watapata ajira na serikali ipate mapato.

Aidha, Kunenge ameiombea mamlaka ya Dawasa kwa kamati ili iweze kutekeleza miradi zaidi ya kuwasaidia wananchi mkoani humo kwakuwa mbali ya uwekezaji pia watu wanaongezeka kila uchwao.