Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mpina awashawishi wabunge wasipitishe bajeti

Mbunge wa Kisesa (CCM), Luhaga Mpina akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria mwaka 2023/2024 leo Aprili 25, 2023 bungeni jijini Dodoma. Picha na Merciful Munuo

Muktasari:

  • Mbunge wa Kisesa (CCM) Luhaga Mpina amelia na upekuzi wa mikataba ya Serikali na kutaka orodha ya mikataba yote iwasilishwe bungeni.

Dar es Salaam. Mbunge wa Kisesa (CCM), Luhaga Mpina amewashauri wabunge wenzie kutopitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka 2023/2024 hadi hapo orodha ya mikataba ya Serikali itakapoletwa bungeni.

 Mpina ameyasema hayo leo Jumanne Aprili 25, 2023 wakati akichangia makadiroo ya mapato na matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria mwaka 2023/2024.

Amesema Mwanasheria Mkuu wa Serikali alifanya upekuzi wa mikataba 1,304 kati 567 yenye thamani ya Sh91 trilioni wakati mikataba 737 haijafanyiwa upekuzi kwa mwaka wa fedha.

“Hajawekwa katika majedwali kwa nini hakuweka, tusipofanya wabunge hivyo Serikali inaweza haipo katika bajeti wala mipango wa maendeleo. Na sisi kama wasimamizi wa mali za Taifa hili tukawa hatujalitendea haki Taifa hili,” amesema.

Amesema hiyo yote ni kujua mikataba hiyo ni ya nini na ya jambo gani.

Mpina amesema hakuna kupitisha ya Wizara ya Katiba na Sheria hadi alepeleke jedwali la mikataba hiyo bungeni.