Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mpina afyatuka bungeni, adai mawaziri wanampikia majungu

Muktasari:

  • “Nataka kuwaambia kwamba hakuna jambo lolote ambalo ninalo ila tuna jambo moja la Watanzania kupata maendeleo. Hakuna hiyana yoyote na huko wanakopeleka majungu, wengine wajue ndio tumekulia,” amesema Mpina.

Dodoma. Mbunge wa Kisesa mkoani Mwanza, Luhaga Mpina amewatuhumu mawaziri kuwa wanampikia majungu kwa kuwa wameshindwa kujibu maswali ama hoja anazozitoa bungeni.

Mpina, ambaye amekuwa na kawaida ya kuzungumza bungeni na kuwachachafya mawaziri, amesema watendaji hao wa Serikali wameshindwa kujibu hoja zake na badala yake wamekuwa wakidai ana jambo lake.

Mpina ameyasema hayo leo Ijumaa, Mei 10, 2024 wakati akichangia mjadala wa kupitisha bajeti ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Maji kwa mwaka wa fedha 2024 / 2025.

“Nataka kuwaambia kwamba hakuna jambo lolote ambalo ninalo ila tuna jambo moja la Watanzania kupata maendeleo. Hakuna hiyana yoyote na huko wanakopeleka majungu, wengine wajue ndio tumekulia,” amesema Mpina.

Endelea kusoma mitandao ya Mwananchi kwa taarifa zaidi