Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mpango kudhibiti rushwa Azaki waja

Muktasari:

  • Changamoto za kukosekana ajenda ya pamoja, msingi wa maadili katika uchechemuzi wa kijamii na upimaji wa matokeo ya kudhibiti vitendo vya rushwa, zimechagiza uandaaji wa mwongozo wa asasi za kiraia.

Dar es Salaam.  Changamoto za kukosekana ajenda ya pamoja, msingi wa maadili katika uchechemuzi wa kijamii na upimaji wa matokeo ya kudhibiti vitendo vya rushwa, zimechagiza uandaaji wa mwongozo wa asasi za kiraia.

 Kutokana na changamoto hiyo, mtandao wa asasi 17 za kiraia chini ya mwamvuli wa Hakirasimali umekutanisha kikundi kazi cha uandaaji wa mpango mkakati wa kuongeza uwazi, uwajibikaji na udhibiti wa rushwa.

Mkakati huo unaandaliwa kwa lengo la kuakisi pia sehemu ya Mpango Mkakati wa Kitaifa wa Kupambana na Rushwa (NACSAP), ambao umekamilika awamu ya tatu 2017/2022.

“Ndio maana asasi za kiraia tumekuwa tukipewa majina mengi,” amesema mshauri elekezi, Kaleb Gamaya leo Agosti Mosi, 2023 wakati wa kikao cha kikundi kazi cha uchambuzi wa rasmu ya mkakati wa asasi hizo ijini Dar es Salaam.

“Hatuna mwelekeo wa pamoja kwenye uchechemuzi kwa mfano wanasiasa, wanaharakati na viongozi wa dini wana njia zao ila sisi tunajikuta tunafuata njia yoyote kati ya hizo,” amesema Gamaya akieleza umuhimu wa mkakati huo.

Kuhusu utekelezaji wa NACSAP, Gamaya amesema mkakati wao utasaidia kujipima kila mwaka katika ushiriki wa kudhibiti rushwa kwa ushahidi wa tafiti mbalimbali ndani ya asasi hizo na kwenye jamii kupitia majukumu yao.

“Kuhusu rushwa, tangu awamu ya kwanza ya NACSAP hatujawahi kuwa na mwongozo kama ilivyo taasisi ya mahakama, Jeshi la Polisi wanaojipima namna gani wameguswa na rushwa kwa mwaka husika, lakini hatuwezi kujipima,” amesema Gamaya.

Kwa mujibu wa Hakirasilimali, kikao hicho chenye zaidi ya wajumbe 50 wakiwamo Bakwata, Policy Forum, Jamii Forum, HakiMadini, taasisi ya WAJIBU, Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Fordia, Takukuru na Wizara ya Nishati.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hakirasikimali, Adam Anthony amesema mkakati huo ulitakiwa kukamilika Februari mwaka huu lakini ulikwama kutokana na changamoto zilizokuwa nje ya uwezo wao.

“Siwezi kusema utakamilika lini lakini unahitaji pia ushirikiano wa taasisi za Serikali katika ukamilifu wake,” amesema Anthony.

Scholastica Jullu, Wakili wa Kampuni ya mbinu za utatuzi wa migogoro (DRM) amesema mpango huo utasaidia jamii kuepuka mitego ya rushwa kuanzia ngazi ya jamii wakati wa utekelezaji wake.