Moto wazuka Ruaha

Muktasari:
- Siku chache baada ya moto kuzuka katika Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro, mwingine umezuka katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha mkoani Iringa na kuteketeza sehemu ya hifadhi hiyo.
Iringa. Siku chache baada ya moto kuzuka katika Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro, mwingine umezuka katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha mkoani Iringa na kuteketeza sehemu ya hifadhi hiyo.
Akizungumza na Mwananchi leo Alhamisi 27, 2022 Mkuu wa hifadhi hiyo, Kamishna Msaidizi wa Uhufadhi, Godwell Meing'ataki amesema kuwa juhudi za kuuzima moto huo uliozuka katika eneo la Ikuka zinaendelea.
Meing'ataki amesema kuwa moto huo umesababishwa na majangili wanaorina asali katika hifadhi hiyo.
Amesema kuwa maofisa uhifadhi wanashirikiana na baadhi ya wananchi wa vijiji jirani kuhakikisha wanaudhibiti moto huo.
Kamishna Msaidizi huyo wa Uhufadhi amesema kuwa athari za moto huo ni kubwa kwa wanyama, wadudu na uoto wa asili.
Baadhi ya vijana waliokuwa wanazima moto huo wamedai kuwa moto huo ulianza siku tatu zilizopita na umetokana na majangili.