Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MKUTANO MAALUM CCM: Madada poa wavamia

Muktasari:

Wasichana hao, ambao Mwananchi imebaini wanatoka katika miji mikubwa kama Dar es Salaam, Arusha, Iringa na Mbeya, wameonekana kwenye maeneo mbalimbali ya starehe wakisaka wanaume nyakati za usiku.

Dodoma. Wasichana wanaofanya shughuli ya kuuza miili, maarufu kama dada poa wameongezeka katika viunga vya mji wa Dodoma tayari kuvizia wageni watakaohudhuria Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM.

Wasichana hao, ambao Mwananchi imebaini wanatoka katika miji mikubwa kama Dar es Salaam, Arusha, Iringa na Mbeya, wameonekana kwenye maeneo mbalimbali ya starehe wakisaka wanaume nyakati za usiku.

Madada poa ambao kwa kawaida hufurika mjini hapa wakati wa vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano, wamekuwa wakiwatoza wateja hadi Sh30,000 kwa ambaye anataka kulala naye hadi asubuhi.  

“Kama unataka madada poa nenda kwenye baa maarufu za mjini hapa nyakati za usiku. Mwanangu mbona mfuko wako tu. Ukitaka wa kulala naye hadi asubuhi, ukitaka wa saa kazi kwako,” alisema mmoja wa wanaume katika moja ya baa maarufu mjini hapa.