Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mila potofu zinavyochangia vifo vya watoto wenye selimundu

Mkurugenzi Mkuu wa Asasi ya Tanzania Sicle Cell Disease Alliance, Dk Deogratias Matanda wakati akizungumza leo Septemba 13, 2024 Jijini Arusha katika kampeni ya kuhamasisha jamii juu ya uchunguzi wa ugonjwa wa selimundu. Picha na Janeth Mushi

Muktasari:

  • Kukosekana elimu ya kutosha kwa jamii na imani potofu vi mambo yanayotajwa kusababisha vifo vya  watoto wao wenye ugonjwa wa selimundu kwa kuwa wengi huwapeleka kwa waganga wa kienyeji badala ya hospitali.

Arusha. Kukosekana kwa elimu ya ugonjwa wa selimundu (sickle cell) nchini Tanzania kumesaabisha baadhi ya wazazi wa watoto wenye ugonjwa huo kuwapeleka kwa waganga wa kienyeji badala ya hospitali na hatimaye kusababisha vifo vyao.

Hali hii imeelezwa kuwa moja ya changamoto kubwa inayopelekea vifo vya watoto wenye umri chini ya miaka mitano kutokana na kukosa matibabu sahihi.

Serikali, kwa kushirikiana na wadau wa afya, imetakiwa kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu ugonjwa huu ili kuongeza uelewa na kuepusha vifo vya watoto.

Haya yameelezwa Ijumaa, Septemba 13, 2024, na mwanaharakati na shujaa wa selimundu, Sanyu Senga, wakati wa kampeni ya kuelimisha jamii kuhusu ugonjwa huo.

Sanyu amebainisha kuwa changamoto kubwa ni kwamba ugonjwa huo haupati sauti ya kutosha nchini, hali inayosababisha imani potofu kwa baadhi ya wazazi kuendelea.

“Baadhi ya wazazi wakigundua watoto wao wana selimundu, badala ya kuwapeleka hospitali, wanawapeleka kwa waganga wa kienyeji au kwenye maombi, wakiamini wataponya bila kuzingatia kuwa ushauri wa kitaalamu,” amesema Sanyu.

AiAmesisitiza umuhimu wa kuhamasisha jamii ili wanapobaini watoto wao wana selimundu, wawapeleke hospitali.

"Mimi ni shujaa wa ugonjwa huu, nina umri wa miaka 47, nina mtoto na haya yote yamewezekana kwa sababu nimepata elimu."

Sanyu alieleza kuwa wamekuwa wakitoa elimu kwa makundi mbalimbali nchini, huku wakitumia mwezi wa Septemba kuhamasisha jamii.

Aliufafanua ugonjwa huo kuwa wa kurithi, ambapo watoto hupata kutoka kwa wazazi wote wawili.


Jinsi ya kuuepuka

Alihimiza utaratibu wa kupima vinasaba kabla ya kuanzisha familia, kama inavyofanyika kwa Virusi vya Ukimwi, ili kuvunja mduara wa urithi wa ugonjwa huo.

Arafa Said, mwanzilishi wa Jumuiya ya Wagonjwa wenye Selimundu Tanzania, alisema lengo ni kuhakikisha wanaongeza uelewa na upatikanaji wa matibabu bora kwa wenye ugonjwa huo.

“Tunajua changamoto tunazopitia, na tuko hapa kuadhimisha mwezi wa kuhamasisha jamii,” amesema, akibainisha kuwa wadau wamewapa ushirikiano kwa kuamua kupanda Mlima Kilimanjaro kwa niaba ya wagonjwa wa selimundu ili kufikisha ujumbe.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Sickle Forward kutoka Marekani, Dk Allan Anderson, ambaye ameongozana na wanaharakati zaidi ya 20, amesema wanapanda Mlima Kilimanjaro ili kukusanya fedha kwa ajili ya wagonjwa wa selimundu katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Dk Allan ameeleza kuwa lengo ni kuongeza utambuzi wa mapema kwa watoto wachanga ili kuanza matibabu haraka, na mpaka sasa wamekusanya zaidi ya Dola za Marekani 1.2 milioni (Sh 3.27 bilioni) kwa ajili ya kusaidia nchi hizo.

Pia wameeleza umuhimu wa kusaidia vitendanishi vya uchunguzi ili kuokoa vifo vya watoto wadogo.

Dk Edna Ntulwe, mratibu wa magonjwa yasiyoambukiza Arusha, amesema zaidi ya watoto 10,000 hugundulika kuwa na selimundu kila mwaka nchini, hivyo ni muhimu elimu ikaendelea kutolewa ili kukata mnyororo wa kuzaliwa watoto wenye ugonjwa huo.

Kwa upande wake Dk Deogratias Matanda, mtendaji mkuu wa Tanzania Sickle Cell Disease Alliance, amesema tatizo hilo bado ni kubwa nchini, ambapo asilimia 70 hadi 90 ya watoto wanaozaliwa na ugonjwa huo hufariki kabla ya kufikisha umri wa miaka mitano, endapo hawatapata matibabu mapema.