Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mikopo 'shavubwebwea' yaongoza kuvunja ndoa Tanga

Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Tanga, Husna Sekiboko

Muktasari:

  • Wakati Benki kuu ya Tanzania (BoT) ikiendelea kusisitiza kuwa ni kinyume cha sheria mtu au taasisi kujihusisha na utoaji wa mikopo bila leseni kutoka benki hiyo, Wakazi wa Tanga wameendelea kuugulia maumivu ya mikopo shavubwebwea inayotolewa kiholela mtaani kwa masharti magumu.  

Tanga. Wanawake wilayani Tanga mjini kata ya Mzingani, Mabokweni na Mnyanjani wameelezea changamoto wanazopitia kurejesha mikopo yenye masharti magumu maarufu kama ‘shavubwebwea’ huku wakiitaja kuwa chanzo cha kuvunjika kwa ndoa zao.

Wameyasema hayo leo Jumapili Julai 30, 2023 mbele ya Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga, Husna Sekiboko katika ziara yake wakati akizungumza na wananchi wa kata hizo.

Mikopo hiyo ni ile wanayochukua asubuhi na kutakiwa kufanya marejesho jioni ‘kausha damu’ na endapo watashindwa kufanya marejesho hupokonywa mali zao.

 “Tunadhalilika vitu vyetu vinachukuliwa na watu, tunaomba Serikali itusaidie kurudisha mikopo tuliyokuwa tunapewa kupitia Halmashauri," amesema Zainabu Shabani mkazi wa Tanga mjini.

Naye Amina Mbwana amesema mikopo hiyo inahatarisha ndoa zao kwani wanashindwa kulea familia kutokana na kufuatwa mara kwa mara.

“Tunashindwa kulea familia zetu sababu muda mwingi tunakimbia majumbani mwetu ili wanapokuja kuchukua marejesho wasitukute,”amesema.

Mikopo ya halmashauri waliyoitaja wananchi hao ni ile ya iliyokuwa ikitolewa na Serikali kwa kundi la vijana wanawake na makundi maalumu ambayo April 13, 2023 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihitimisha hoja yake ya makadirio ya maombi na matumizi ya fedha kwa mwaka 2023/24 alieleza dhamira ya Serikali kusitisha utoaji wa mikopo hiyo.

Akizungumza na wananchi hao Husna amesema Serikali inafanya utaratibu wa kuendelea kutoa mikopo hiyo kwa makundi hayo.

Mbunge huyo amesema kilichosababisha mikopo hiyo kuondolewa ni ni wizi na udanganyifu uliokuwa ukifanywa na baadhi ya watu kwa kutengeneza vikundi hewa.

"Tuvute subra serikali yetu ichakate ili ije na mpango mzuri mikopo itolewe na iende Kwa wale walengwa waliokusudiwa,"amesema Sekiboko.

Hata hivyo ametoa angalizo kuwa endapo mikopo itaanza kutolewa basi walengwa watumie kufanya shughuli zitakazoleta tija ili uweze kurejesha na wengine Waze kukopesheka badala ya kutomia mikopo hiyo kwenda kununua vijora au kwenda kuongeza wanawake (kuoa).

Kuhusu mikopo kausha damu, tayari Benki kuu ya Tanzania (BoT) imepiga marufuku watu au taasisi kujihusisha na biashara ndogo za huduma za fedha bila kuwa na leseni ya benki hiyo au taasisi zilizokasimishwa majukumu hayo.

BoT ilifafanua kuwa kufanya kitendo hicho ni kinyume na kifungu cha 16(1) cha sheria ya huduma ndogo za fedha ya mwaka 2018.