Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mikoa kinara kilimo cha bangi hii hapa

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama akizungumza na vyombo vya habari bungeni jijini Dodoma, baada ya kuwasilisha bungeni taarifa ya hali ya dawa za kulevya ya mwaka 2022 leo. Picha na Merciful Munuo

Muktasari:

  • Wakati wafanyabiashara wa dawa za kulevya wakibuni njia mpya ya kuweka bangi katika vyakula, mikoa sita inayolimwa bangi hiyo kwa wingi yatajwa.

Dodoma. Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Jenista Mhagama ametaja mikoa sita inayolimwa bangi kwa wingi nchini ikiwa ni pamoja na Arusha.

Mikoa mingine ni Iringa, Morogoro, Manyara ambayo imekuwa ikilima bangi kwa ajili ya kuuza nje ya nchi huku Mara na Ruvuma ikilima kwa matumizi ya ndani.

Mhagama ameyasema hayo leo Mei 30, 2023 baada ya kuwasilisha bungeni taarifa ya hali ya dawa za kulevya ya mwaka 2022.

Amesema hivi karibuni, kumeibuka tabia ya kuchanganya bangi yenye kiasi kikubwa cha kilevi kwenye vyakula kama vile biskuti, asali, juisi, majani ya chai na keki.

Amesema waliwakamata watu wawili mtu na mke wake mkoani Arusha kwa kukutwa wakitengeneza biskuti, keki na asali zikiwa zimechanganywa bangi.

Mhagama amesema bidhaa hizo zilikuwa zimefungashwa kwa ajili ya kusafirishwa kwenda nje na kwamba watu hao wameshahukumiwa kifungo cha miaka 30.

Amesema pia wanaendelea na uchunguzi wa kiwanda cha biskuti ambacho kinadaiwa kutengeneza biskuti ambazo zimechanganywa na bangi.