Mbwa anauzwa Sh 3milioni Sabasaba

Muktasari:
Amesema kwa hapa nchini, wanauzwa kuanzia Sh 3milioni.
Dar es Salaam. Moja ya vivutio vilivyo katika maonyesho ya kimataifa ya biashara (Sabasaba), ni mbwa wanaouzwa kati ya Sh1 milioni hadi Sh3 milioni.
Mbwa hao wapo katika banda la kampuni ya Safia Dog Kennelly.
Banda hilo lina mbwa wa aina sita, ambao wamegeuka kivutio zaidi kwa watazamaji wa maonyesho hayo.
Ofisa Masoko wa kampuni hiyo, Sylvester Luena ammesema mbwa hao ni mahsusi kwa ajili ya ulinzi wa nyumbani na ofisini, au taasisi.
Amewataja baadhi ya mbwa hao kuwa ni American Bully anayetajwa kuwa mkali na anashambulia kama simba.
“Huyu ni mkubwa, msikivu na mkali sana, anashambulia kama simba,” amesema
Amesema kuna mbwa anaitwa French Mastiff, Boa Bully toka South Afrika, American Bully na Cannecorso.
Mbwa hawa wanasifa za kiutendaji zinazofanana lakini wana maumbile tofauti.
Amesema kuna mbwa aina ya ‘English dog’ hawa ni wapole kupita kiasi wanatumika zaidi kama mapambo ya nyumbani lakini wanauzwa bei ghali kuliko mbwa yeyote duniani,” amesema
Amesema kwa hapa nchini, wanauzwa kuanzia Sh 3milioni.