Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbowe akutana na Balozi wa Marekani, wajadili demokrasia

Muktasari:

  • Hii si mara ya kwanza kwa wawili hao kukutana, Novemba 3, 2023 walikutana na Mbowe aliandika katika ukurasa wake wa X kuwa miongoni mwa mengi waliyojadili ni changamoto kadhaa zinazokabili ujenzi wa demokrasia nchini Tanzania.

Dar es Salaam. Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Michael Battle amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe.

Wawili hao wamejadili masuala ya mabadiliko ya kidemokrasia nchini Tanzania, kwa mujibu wa Balozi Battle aliyeandika ujumbe katika ukurasa wake wa X (zamani Twitter).

“Nimefurahi kuungana tena na Freeman Mbowe kujadili maendeleo ya mabadiliko ya kidemokrasia nchini Tanzania,” ameandika Balozi Battle.

Mbowe amekutana na Balozi Battle ikiwa zimepita siku chache tangu alipotangaza  kufanyika kwa maandamano nchi nzima Januari 24, 2024 kushinikiza Serikali kuondoa miswada mitatu ya sheria za uchaguzi alizodai haijazingatia maoni ya wananchi.

Hii si mara ya kwanza kwa wawili hao kukutana, Novemba 3, 2023 walikutana ambapo Mbowe katika ukurasa wake wa X aliandika akieleza kwamba miongoni mwa mengi waliyojadili, ni changamoto kadhaa zinazokabili ujenzi wa demokrasia nchini Tanzania.

Pia, amemshauri kuhusu umuhimu wa kuendeleza juhudi shirikishi zitakazowezesha ujenzi wa demokrasia imara itakayoweka misingi ya maendeleo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii nchini Tanzania.

Aidha, amemueleza Balozi hofu yake kuhusu uharibifu wa mazingira katika Mlima Kilimanjaro na mfumo wake wa ikolojia.