Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mabalozi wanaohudhuria kesi ya Mbowe waonywa

Mabalozi wanaohudhuria kesi ya Mbowe waonywa

Muktasari:

  • Waziri Mulamula amewataka mabalozi wanaokwenda mahakamani kufuatilia mwenendo ya kesi ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kufuata sheria na taratibu za kidiplomasia.


Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula amewataka mabalozi wanaokwenda mahakamani kufuatilia mwenendo ya kesi ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kufuata sheria na taratibu za kidiplomasia.

Balozi Mulamula ameyasema hayo leo Ijumaa Agosti 20,2021 jijini Dar es Salaama wakati akizungumza na mabalozi, wakuu wa taasisi na mashirika ya kimataifa mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc) uliofanyika Lilongwe, Malawi Agosti 17–18.

Katika mkutano huo, Balozi Mulamula amesisitiza kwamba mabalozi wanaokwenda mahakamani kufuatilia mwenendo wa kesi ya Mbowe kufuata sheria na taratibu za kimataifa za kidiplomasia ili kujiepusha na ukiukwaji wa sheria na taratibu hizo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mulamula amesema Serikali haina lengo la kuwazuia mabalozi hao kwenda mahakamani.

Hata hivyo, taarifa hiyo imesema kutokana na  uwepo wa janga la Uviko-19 pamoja na msongamano ni muhimu kuchukua tahadhari ikiwa ni pamoja na kufuatilia shauri hilo kwa njia nyingine ikiwemo kupitia vyombo vya habari.

“Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ndiyo yenye jukumu la kuhakikisha usalama wa wanadiplomasia waliopo hapa nchini. Hata hivyo, kwa siku za hivi karibuni baadhi ya wanadiplomasia hao wameonekana mahakamani bila kufuata sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia masuala ya Kidiplomasia ikiwemo kutoa taarifa kwa Wizara ya Mambo ya Nje,” amesema Balozi Mulamula katika taarifa hiyo.


Kwa upande wake, kiongozi wa mabalozi waliopo hapa nchini, Dk Ahamada El Badaoui alisema ulinzi wa mabalozi waliopo hapa nchini ni muhimu na endapo kuna mabalozi wanafanya hivyo ni vyema wakafuata taratibu na sheria zilizopo.

Akizungumza na gazeti hili, mjumbe wa Umoja wa Ulaya hapa nchini ambaye hakutaka jina lake litajwe, amesema wamepokea tahadhari kutoka serikalini kwa wanadiplomasia.

“Tulihudhuria usikilizwaji wa kesi inayomkabili kiongozi wa chama cha upinzani, Freeman Mbowe kwa sababu ni haki yetu kama mabalozi kufuatilia hali ya kisiasa katika nchi ambayo tumo wakati huo.”