Mbowe afiwa na kaka yake, mikutano yaahirishwa

Muktasari:
- Katibu wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema amesema mikutano ya hadhara ya mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe ameahirishwa baada ya kufiwa na kaka yake, Alfred
Moshi. Katibu wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema amesema mikutano ya hadhara ya mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe ameahirishwa baada ya kufiwa na kaka yake, Alfred.
Alfred amefariki dunia leo Jumapili Julai 28, 2019 ikiwa ni siku moja kabla ya Kiongozi huyo wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuanza ziara ya mikutano ya hadhara hadi Agosti 1, 2019 katika jimbo lake la Hai.
“Kutokana na msiba huu tunalazimika kuahirisha vikao vya ndani na mikutano ya hadhara iliyopangwa kufanyika kwa wiki nzima, na tayari tumetoa taarifa za kuahirishwa kwa mikutano hiyo kwa mamlaka husika. Tutapanga kuifanya baadaye,” amesema Lema.
Katibu huyo amewataka wananchi wa kada mbalimbali kujitokeza kumfariji Mbowe.