Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbegu, mayai ya uzazi biashara inayokua kwa kasi Kenya

Mbegu, mayai ya uzazi biashara inayokua kwa kasi Kenya

Muktasari:

  • Miaka michache iliyopita kununua na kuuza mbegu na mayai ya uzazi lilikuwa jambo lisilofahamika nchini Kenya.

Kenya. Miaka michache iliyopita kununua na kuuza mbegu na mayai ya uzazi lilikuwa jambo lisilofahamika nchini Kenya.

Ila kwa sasa imekuwa biashara inayokua kwa kasi kwa wenza wanaoshindwa kupata mimba na wanawake ambao hawajaolewa wakitafuta watoto kupitia njia ya urutubishaji wa mayai nje ya mwili (IVF), ambapo mbegu na yao hurutubishwa maabara na kuwekwa kwenye tumbo la uzazi.

Nchini Kenya, wanaume sasa wameamua ni wakati wa kuwa watoaji wa mbegu na wanawake wakichagua kuwa watoaji wa mayai.

Mtaalamu wa tiba aliwahi kutania kwamba, “hii itaepusha nafasi ya mwanamke kuchukua mtoa shahawa anayefanana na mwanaume waliyeachana au rafiki yake wa siri.”

Kwa mkupuo mmoja wa mbegu kwa mwanaume wa Kenya hulipwa kati ya Sh3,000 za Kenya (sawa na Sh65,000) hadi Sh10,000 (karibu Sh217,000).

Wanaume katika eneo la Afrika Mashariki kwa mfano Tanzania wanapata Ksh10,000 kama fidia. Ikiwa mwanaume wana sifa nzuri zaidi fidia hufikia hadi Ksh25,000 na Ksh30,000 (Sh651,000).

Kwa sifa chache ambazo mtoa mbegu kama vile kuwa na macho ya kijani au ya njano, ngozi nyeupe, mwili na nywele za kupendeza na akili nyingi, ndiyo sifa zinazoangaliwa kwa malipo mazuri.