Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbaroni kuwaua baba, baba mdogo na kuwazika mbele ya nyumba

Muktasari:

  • Polisi Dar es Salaam inamshikilia Hosamu Hamza kwa tuhuma za kuwaua baba na baba mdogo na kuwagfukia mbele ya nyumba.

Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linamshikilia Hosamu Hamza, maarufu Maopena, kwa tuhuma za kuwaua baba yake mzazi pamoja na baba yake mdogo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo, Jumamosi Julai 18, 2026, na Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Faustine Mafwele, mtuhumiwa alikamatwa jana Julai 17 majira ya saa 9 alasiri katika eneo la Makongo akiwa na kisu kilichokuwa na madoa ya damu, huku mavazi aliyokuwa amevaa pia yakiwa na alama za damu.

“Wakati mahojiano yakiendelea, Jeshi la Polisi lilipokea taarifa kutoka kwa wananchi kuhusu kutoweka kwa watu wawili waliokuwa wakiishi katika nyumba moja iliyopo Mtaa wa Sindano, Mwananyamala, huku damu zikionekana ndani ya nyumba hiyo.

“Uchunguzi uliofanywa na wataalamu wa uchunguzi wa kisayansi ulibaini miili ya watu wawili waliotambuliwa kuwa Hamza Juma Omari, maarufu Mautila (48), na Ally Juma Omari (37),” ameeleza Mafwele.

Katika taarifa hiyo, Mafwele amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa mtu aliyefanya tukio hilo la mauaji na kuwafukia marehemu hao ni Maopena, ambaye ni mtoto wa marehemu Hamza Juma Omari, maarufu Mautila.

Mafwele amesema sababu halisi zilizomfanya mtuhumiwa kutekeleza tukio hilo bado zinaendelea kuchunguzwa na Jeshi la Polisi.


Simulizi ya familia

“Nilijikaza moyo kushuhudia ndugu zangu wakifukuliwa, lakini nilichokiona siwezi kukisahau maishani. Walikuwa wameuawa kikatili na kufukiwa. Hatujui walifanyiwa nini kabla ya kuuawa, lakini kwa sasa tunachoomba ni haki itendeke,” amesema dada mkubwa wa familia, Mwanahamisi Omary.

Kauli hiyo inaakisi maumivu yanayoikabili familia ya Omary baada ya kupoteza ndugu zao wawili, Ally Omary, maarufu Bob, aliyekuwa kondakta wa daladala za Masaki–Simu 2000, na kaka yake, Hamza Omary, maarufu King Hamza, aliyekuwa akijishughulisha na biashara ya kukusanya makopo ya plastiki.

Akizungumza na Mwananchi leo, Julai 18, 2026, Mwanahamisi amesema walipoteza mawasiliano na ndugu hao usiku wa kuamkia Julai 17 mwaka huu baada ya simu zao kutopatikana, jambo ambalo halikuwa la kawaida.

"Tulikuwa tunawapigia simu lakini hazikupatikana. Hilo halikuwa jambo la kawaida kwao. Ndipo tukaanza kuwa na hofu. Baada ya muda nikapigiwa simu niambiwe nifike hapa nyumbani kwa sababu kuna tatizo. Nikawaambia waniweke wazi kama kuna msiba, nikihisi Ally amefariki kwa sababu hakuwa anapatikana," amesema Mwanahamisi.

Kuhusu chanzo cha tukio hilo, Mwanahamisi amesema bado hawana majibu ya uhakika. Hata hivyo, amesema kabla ya tukio Hosamu alikuwa akidai nyumba hiyo ni urithi alioachiwa na babu yake na kutaka kuishi humo pamoja na mpenzi wake.

Amesema madai hayo hayakuwa ya kweli, kwa kuwa suala la umiliki wa nyumba hiyo halikuwa kama mtuhumiwa alivyokuwa akidai.

"Kuna siku huyu kijana alisema nyumba hii aliachiwa na babu yake kama urithi kabla hajafariki, jambo ambalo limetushangaza. Tangu baba yetu aanze kuugua hadi anafariki, huyu kijana hakuwepo. Ndiyo maana tunashangaa anapodai aliachiwa nyumba hiyo kama urithi," amesema.

Naye, Husna Omary, ambaye ni shangazi wa mtuhumiwa Hosamu, amesema kabla ya tukio hilo la mauaji kijana huyo alikuwa akijihusisha na matumizi ya bangi baada ya kurejeshwa kutoka Afrika Kusini Julai 2025.

"Hosamu tumemlea sisi wenyewe hapa. Baadaye alichukuliwa na mjomba wake kwenda Afrika Kusini. Alirudishwa mwaka jana na akaenda kuishi kwa mama yake Gongo la Mboto. Kutokana na vituko alivyokuwa akimfanyia mama yake na baba yake wa kambo, alifukuzwa saa 10 alfajiri, kisha akarudi hapa baada ya miezi miwili tu," amesema Husna.