Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mataifa Afrika yatakiwa kutenga fedha kupambana na malaria

Mwenyekiti wa Taasisi ya Muungano wa Viongozi wa Afrika katika Kudhibiti Malaria (ALMA), ambaye pia ni Rais wa Guinea Bissau, Umaro Embaló (katikati) alipotembelea miradi mbalimbali nchini, katika ziara yake ya siku tatu.

Muktasari:

  • WHO imetahadharisha kuwa bila hatua za haraka, malaria itaendelea kuwa tishio kubwa.

Dar es Salaam. Mataifa ya Afrika yametakiwa kuhakikisha yanatenga sehemu ya bajeti zake za ndani kwa ajili ya kutokomeza ugonjwa wa malaria.

Wito huo unakuja katika kipindi ambacho Shirika la Afya Duniani (WHO) limeiweka Tanzania katika nafasi ya 10 kwa nchi zinazokabiliwa na ugonjwa huo tangu mwaka 2020.

Kuwepo kwa Tanzania katika nafasi hiyo, kumetokana na idadi ya vifo vinavyosababishwa na malaria kuwa 21,758 sawa na asilimia 7.38 kwa mwaka 2020. Hiyo ni sawa na wastani wa vifo 48.99 kwa kila vifo 100,000.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Taasisi ya Muungano wa Viongozi wa Afrika katika Kudhibiti Malaria (ALMA), ambaye pia ni Rais wa Guinea Bissau, Umaro Embaló alipotembelea kituo hicho jijini Dar es Salaam.

Embalo amesisitiza hatua hiyo inatishia linatishia kuvuruga utoaji huduma muhimu za kuokoa maisha kutokana na ugonjwa wa malaria kurudisha nyuma mafanikio ya miongo kadhaa.

“Kuna uhitaji wa haraka kwa nchi kuchukua hatua, ili kupunguza athari mbaya zinazotokana na mgogoro wa kifedha duniani, kuongezeka kwa usugu wa viatilifu na dawa za kutibu malaria, mabadiliko ya hali ya hewa na madhara ya kibinadamu,” amesema.

Ameeleza iwapo hali hiyo itaendelea kupuuzwa katika kipindi cha miaka 20 ijayo kutakuwa na hali mbaya zaidi juu ya mlipuko wa ugonjwa huo.

Amesisitiza nchi zinatakiwa kuhakikisha zinatenga fedha katika bajeti kutoka vyanzo vya ndani, ili kutokomeza ugonjwa huo.

Kwa mujibu wa WHO, tangu mwaka 2015, kasi ya maendeleo katika kupunguza wagonjwa wapya na vifo vitokanavyo na malaria imepungua katika nchi kadhaa za Afrika.

Kadhalika, mwenyekiti huyo amezitaka nchi nyingine za Afrika kuanzisha mabaraza na mfuko wa kutokomeza malaria, huku pia ikichangia rasilimali za ndani hasa kutoka sekta binafsi kama inavyofanyika Tanzania na Guinea Bissau.