Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Marekani kuweka kituo cha karantini Kenya kwa raia wake wanaoshukiwa kuugua Ebola

Picha na Mtandao.

Muktasari:

  • Kituo kilichopendekezwa kitatumiwa kuwaweka Wamarekani walio katika hatari kubwa ya kuambukizwa aina hatari ya Ebola ya Bundibugyo, inayoenea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Uganda.

Dar es Salaam. Marekani inakusudia kujenga eneo la karantini na matibabu kwa raia wake nchini Kenya, watakaogundulika kuwa na ugonjwa wa Ebola nchini DRC Congo.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu ya Marekani White House Mei 27, 2026, kituo hicho kinakusudiwa kuhakikisha Wamarekani wanaohitaji kuondoka haraka DRC wanapata huduma bora za afya na sehemu salama ya kujitenga, bila kulazimika kusafirishwa kwenda Marekani.

Kituo hicho kitatoa matibabu ikiwemo huduma za wagonjwa mahututi na mgonjwa kufanyiwa tathmini kama anahitaji kuhamishiwa eneo lingine kwa matibabu ya juu zaidi, ili kuongeza nafasi ya kupona.

Tarifa hiyo ya Ikulu, haikueleza wazi kama Wamarekani wataruhusiwa kurejea Marekani ikiwa hawatataka kwenda Kenya.

Kwa sasa, Marekani imewapiga marufuku watu wenye Green Card (kibali cha ukaazi nchini humo) waliotembelea hivi karibuni DRC, Uganda na Sudan Kusini kurejea nchini humo pamoja na wasafiri wengine waliotembelea nchi hizo tatu hawataruhusiwa kuingia ndani ya taifa hilo.

Akizungumzia hatua hiyo, Mtaalamu wa Magonjwa ya mlipuko na Mkurugenzi wa Kituo cha Magonjwa ya Mlipuko Chuo Kikuu cha Brown University School of Public Health, Jennifer Nuzzo amesema anashangazwa na uamuzi wa utawala wa Marekani.

 “Kinachonishangaza ni kuona Serikali ikitafuta njia ya kuwazuia Wamarekani kurejea nyumbani kupata huduma bora za kitabibu ambazo vituo vyetu vya matibabu na udhibiti wa magonjwa tayari vina uwezo wa kutoa,” amesema Nuzzo.

Mtaalamu huyo amesema upo uwezekano wa mtu kushindwa kurudi nyumbani kupata matibabu salama na yenye ufanisi, hivyo kuwafanya baadhi ya watu wasitoe taarifa kwamba wameathirika, hali itakayoongeza hatari ya kusambaa ugonjwa huo kwa siri.

“Hii ni sawa na kuwaambia wahudumu wa afya wa Marekani watakaoenda kusaidia kukabiliana na mlipuko huu wakiumwa hawataruhusiwa kurudi nyumbani,” amesema Jeremy Konyndyk, Rais wa Kituo cha Kimataifa cha Wakimbizi (Refugees International) ambaye pia amewahi kuwa kiongozi wa kikosi kazi cha UVIKO-19 cha USAID.

Wataalamu hao wanaeleza kuwa hatari ya usafirishaji wa mtu aliyeathirika na Ebola ni ndogo sana, ikiwa mtu huyo bado hajaonyesha dalili za ugonjwa.

Wamesema Marekani ina uzoefu mkubwa wa kuwahamisha watu waliokaribiana na wagonjwa wa Ebola au waliothibitika kuwa na maambukizi ya Ebola pamoja na magonjwa mengine ya kuambukiza.

Kulingana na Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Marekani (CDC), nchini Congo kunashukiwa kuwa na maambukizi ya watu 906 wenye maambukizi ya Ebola ikiwa ni pamoja na 105 waliothibitishwa, huku vifo 223 vikihusishwa na ugonjwa huo.

Shirika la Habari la Reuters linaeleza raia saba wa Marekani wamepata maambukizi ya Ebola akiwamo daktari mmoja aliyetambulika kuwa mmishenari wa matibabu Peter Stafford.

Mtaalamu huyo aliambukizwa Ebola alipokuwa akifanya kazi nchini DRC na kupelekwa Ujerumani kwa matibabu.

Wamarekani wengine sita walio katika hatari kubwa pia, wamehamishiwa Ujerumani na Jamhuri ya Czech kwa ufuatiliaji na uchunguzi.