Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Malembo atoa darasa la kilimo chenye tija

Muktasari:

  • Wadau wa kilimo wametaja baadhi ya vitu vinavyopaswa kuzingatiwa ili kudhibiti mfumuko wa bei ikiwemo upatikanaji wa mbegu bora na kuangalia afya ya udongo kabla ya kulima.

Dar es Salaam. Mdau wa kilimo ameshauri njia zinazoweza kutumika katoka kudhibiti mfumko wa bei nchini ikiwemo kuboresha maslahi ya wakulima.

Pia, ameshauri wakulima wapewe mbegu bora, afya ya udongo na maji viangaliwe na iangaliwe namna ya kudhibiti wadudu.

Hayo yalisemwa leo Jumatano Februari 8, 2023 katika mjadala kwa njia ya Twitter (Twitter Space) ulioratibiwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, uliohusu ‘Serikali imechukua hatua kukabiliana na mfumuko wa bei, nini maoni yako'.

Mjadala umehusisha wakulima, wananchi na viongozi wa Serikali akiwemo, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba.

Emmanueli Kimaro ambaye ni mdau wa Kilimo amesema upatikanaji mbegu, kuangalia afya ya udongo ni vitu vinavyochukuliwa kirahisi lakini vina matokeo makubwa.

Ametolea mfano wa mahindi, kama nchi inatumia hekta milioni 6.7 lakini mahitaji ya mbegu bora ni changamoto kwa wakulima.

Amesema mahitaji ya mbegu bora ni kama tani 151,969 lakini usambazaji ni takribani tani 41,000.

"Hawa wakulima pia wanatakiwa wapate wataalamu wa kuwatembelea,” amesema

Amesema ni vyema pia kuangalia mbadala wa namna ya kulima badala ya kutegemea mvua kwa kile alichokieleza katika baadhi ya maeneo ukame ulikuwa umeathiri kwa kiasi kikubwa.
"Ni vyema pia wakulima wahamasishwe kupanda mazao yanayoweza kuhimili hali ya ukame kama viazi," amesema Kimaro.

Lucas Malembo ambaye ni mshauri wa masuala ya kilimo biashara amesema tija katika kilimo ni ndogo ambayo inafanya ardhi kubwa kutumika kuzalisha kitu kidogo.

"Waziri wa kilimo inasisitiza sana neno tija katika kilimo na wakulima wasiitwe wadogo bali wafanyabiashara naunga mkono. Ukiangalia takwimu za NBS hekta moja ya mahindi inatakiwa izalishe wastani wa tani sita lakini hadi sasa tunazalisha wastani wa tani 1.5.

Katika mpunga NBS inaonyesha hekta moja inatakiwa ikupe wastani wa tani 6 lakini hadi sasa mkulima anapata wastani wa tani 1.5.

"Utagundua sasa hivi uzalishaji wa mazao unasaidia kupunguza mfumuko wa bei kwa asilimia 59 na tunazalisha lakini si kwa tija, tafsiri yake ni kuwa hili tatizo litaendelea kuwepo na kuwepo,” amesema.