Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Majeruhi wa ajali iliyoua watano Sikonge waruhusiwa

Muktasari:

Majeruhi 13 kati ya 48 wa ajali ya basi la Sasebosa iliyotokea wilayani Sikonge jana jioni wameruhusiwa kutoka hospitali baada ya kupatiwa matibabu na afya zao kuimarika.

Tabora. Majeruhi 13 kati ya 48 wa ajali ya basi la Sasebosa iliyotokea wilayani Sikonge wameruhusiwa kutoka hospitalini baada ya kupatiwa matibabu na afya zao kuimarika.

Ajali hiyo ilitokea jana Ijumaa Julai Mosi, 2022 jioni katika kijiji cha Mabangwe wilayani Sikonge mkoani Tabora na kusababisha vifo vya watu watano.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao amesema basi hilo lilikuwa linatoka mkoani Mbeya kwenda Tabora.

Kwa mujibu wa mganga mfawidhi Hospitali teule ya Sikonge, Dk Peter Songoro amesema majeruhi 29 bado wapo katika Hospitali ya Wilaya ya Sikonge, watano wamepelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora, Kitete huku mmoja akipelekwa katika Hospitali ya Malolo.

Katika Vifo vilivyotokea mwanaume ni 1 wanawake 3 na mtoto mmoja wa kike.

Chanzo cha ajali hiyo kinaelezwa kuwa ni kupasuka kwa tairi la mbele la basi hilo.

Ajali hiyo imetokea Jana jioni katika Kijiji hicho lililosababisha basi la Sasebosa lililotokea Mbeya kwenda Tabora kusababisha vifo hivyo na majeruhi hao.