Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watano wafa ajalini, 17 wajeruhiwa Tabora

Muktasari:

  • Watu watano wamefariki dunia na wengine 17 kujeruhiwa katika ajali ya basi iliyotokea jana Ijumaa jioni Julai Mosi, 2022 katika kijiji cha Mabangwe wilayani Sikonge mkoani Tabora.


Tabora. Watu watano wamefariki dunia na wengine 17 kujeruhiwa katika ajali ya basi iliyotokea jana Ijumaa jioni Julai Mosi, 2022 katika kijiji cha Mabangwe wilayani Sikonge mkoani Tabora.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora, Richard Abwao amesema basi hilo la Sasebosa lilikuwa linatoka mkoani Mbeya kwenda Tabora.

Kamanda Abwao amesema majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa katika hospitali ya Rufaa mkoani hapo kwa ajili ya matibabu.