Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Majeruhi ajali Kigoma wapelekwa Bugando

Kigoma. Majeruhi wa watatu wa ajali iliyotokea barabara ya Kibondo-Kakonko iliyohusisha gari aina ya Toyota Probox lililogongana na gari ya kampuni ya ujenzi ya barabara ya Chiko, wamepewa rufaa kwenda katika hospitali ya Bugando kwa matibabu zaidi.

Ajali hiyo iliyotokea Desemba 23, 2023, saa 11.30 jioni katika kijiji cha Mumkungwa, Kata ya Misenzero barabara ya Kibondo-Kakonko na kusabaisha vifo vya watu wanane huku wengine sita kujeruhiwa.

Akizungumza jana Mganga wa Mkuu wa hospitali ya Wilaya ya Kibondo (DMO) Henry Chinyuka alisema majeruhi watatu wamesafirishwa kwenda hospitali ya Bugando kwa matibabu zaidi.

Aliwataja waliosafirishwa ni Sylvanus Mibala(48),Sara Bundala(20) na Dorice Bundala(22) kwaajili ya matibabu zaidi baada ya kuumia sana.

Alisema majeruhi watatu waliobakia katika hospitali ya Wilaya ya Kibondo hali zao zinaendelea vizuri.

Majeruhi hao ni Flavianus Felician(28), Daniel Samwel (38) na Juma Said(27).

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Thobias Andengenye alisema miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya Wilaya ya Kibondo kwa uchunguzi na kwamba chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa madereva wote ambapo dereva wa Probox alitaka kupita gari lililokuwa mbele yake kwenye kona.

“Nitoe wito kwa watumiaji wa vyombo vya moto, wahakikishe wanachukua tahadhari wanapokuwa barabarani kwa kipindi hiki cha msimu wa sikukuu” alisema na kuongeza:

“Tunaamini tukishirikiana kila mmoja wetu tutafanikiwa kutokomeza ama kupunguza kabisa ajali ambazo sababu zake kimsingi ni uzembe wa madereva,” alisema RC Andengenye.