Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mahakama yatoa amri kesi ya Lissu

Muktasari:

  • Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tundu Lissu imeahirishwa hadi Julai 15, 2025 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imetoa amri kwa Serikali kuhakikisha inatoa uamuzi haraka katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu ili kama wana ushahidi wa kumshtaki ashtakiwe au kama hawana ushahidi asiendelee kukaa gerezani.

Uamuzi huo umetokewa leo, Jumanne Julai Mosi, 2025 na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Franco Kiswaga wakati kesi hiyo ya uhaini ilipoitwa kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Kiswaga amefikia hatua hiyo, baada ya Serikali kuieleza mahakama jalada la kesi hiyo limeshasomwa na kutolewa uamuzi wa kisheria na kwa sasa lipo tayari kwa ajili ya kutolewa uamuzi.

Hata hivyo, kabla ya kutolewa uamuzi huo, Lissu alitoa maombi mawili, moja kama upande wa mashtaka wanao ushahidi wa kutosha basi wasajili taarifa muhimu Mahakama Kuu ili kesi hiyo ihamishiwe huko na kama wameona hakuna ushahidi wa kutosha waifute chini ya kifungu namba 91(1) cha Sheria cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), sura ya 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2022.

"Mheshimiwa hakimu kama upande wa mashtaka wanao ushahidi wa kutosha basi wasajili taarifa muhimu Mahakama Kuu ili kesi hii iweze kuhamishiwa huko au kama hawana ushahidi wa kutosha basi DPP aite Nolle Prosequis (kusitisha mashtaka dhidi ya mshtakiwa," amesema Lissu.

Lissu alitoa maombi hayo, baada ya kiongozi wa jopo la mawakili watano wa Serikali, Nassoro Karuga kueleza mahakama hiyo kuwa kesi hiyo iliitwa kwa ajili ya kutajwa na tayari jalada la kesi hiyo limeshasomwa na kutolewa uamuzi wa kisheria, hivyo wanaomba wapangiwe tarehe nyingine kwa ajili ya kutolewa uamuzi.

Hakimu Kiswaga baada ya kutoa uamuzi huo ameahirisha kesi hiyo hadi Julai 15, 2025 itakapotolewa uamuzi na upande wa mashtaka.


 Endeela kufuatilia mitandao ya kijamii ya Mwananchi