Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mahakama Kuu kutoa uamuzi maombi ya Lissu Julai 11, 2025

Dar es Salaam. Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam imepanga kutoa uamuzi wa maombi ya Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, Julai 11, 2025.

Lissu amefungua shauri la maombi mahakamani hapo akipinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam, Kisutu kuahirisha usikilizwaji wa kesi ya kuchapisha taarifa za uwongo mtandaoni, ulioyolewa Juni 2, 2025.

Katika maombi hayo Lissu anaiomba Mahakama Kuu ilitie jalada la kesi hiyo ya jinai inayomkabili Kisutu ili ichunguze na kujiridhisha, pamoja na mambo mengine uhalali na usahihi wa mwenendo wa kesi hiyo kwa tarehe hiyo.

Hata hivyo, Seikali imeweka pingamizi hoja hiyo ikiiomba mahakama itupilie mbali maombi yake ikiwasilisha sababu sita.

Katika sababu hizo Seriali imedai kuwa maombi hayo yanakiuka kifungu cha 372(2) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, kinachozuia rufaa au mapitio dhidi ya uamuzi au amri ya mahakama isiyomaliza shauri la msingi.

Nyingine ni kuwa Serikali inadai mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza maombi hayo kulingana na moja ya mambo anayoyaomba ambayo yanalenga kuifanya mahakama iangalie kama kifungu cha 188 cha sheria hiyo kinakiuka ama hakikiuki Katiba.

Sababu nyingine iliyowasilishwa na Serikali ni kuwa maombi ya Lissu ni batili kwa kujumuisha mambo tofauti tofauti kwa pamoja.

Hata hivyo, timu ya mawakili wa Lissu imepinga hoja za pingamizi hilo wakidai hazina mashiko na kwamba, shauri hilo liko sawa na halijakiuka sheria huku wakisisitiza kuwa mahakama hiyo ina mamlaka ya kulisikiliza.

Jaji Elizabeth Mkwizi ameahirisha shauri hilo hadi Julai 11, 2025 kwa ajili ya uamuzi.

Mara baada ya kuahirishwa kwa shauri hilo, Lissu akiwa anatoka alikutana na wafuasi wa Chadema ambao, walisikika wakiinadi kampeni ya no reforms, no election ambapo, naye aliijibu huku akisema kikao kinaendelea.