Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Madereva wa malori wanaosafirisha madini kutoka DRC wagoma

New Content Item (1)

Muktasari:

  • Madereva wa malori yanayosafirisha shaba na madini mengine kutoka migodi ya DRC, wameingia kwenye mgomo wa siku 10 sasa kushinikizwa kulipwa malipo ya fidia ya hatari katika kusafirisha raslimali hiyo kuja nchini.

Dar es Salaam. Madereva wa malori wanaosafirisha rasilimali ya madini ya shaba, kopa na kobalt kutoka migodi ya  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuja nchini wameingia kwenye mgomo kushinikiza kulipwa malipo ya fidia ya hatari katika kazi (Risk Allowance).

Katika mgomo huo ambao ukomo wake haujulikani, madereva wanataka walipwe malipo hayo kwa kuwa kubeba raslimali hiyo njiani wanapata changamoto kubwa za kiusalama katika kuilinda na wakiibiwa wabosi wao huwa wanawageuka kuwakata mishahara au kuwapeleka mahakamani kulipa  gharama na wakishindwa baadhi yao wanafungwa.

Sakata hilo linajitokeza ikiwa mwezi mmoja umepita tangu kuripotiwa kwa malori 250 kuzuiliwa DRC, kutokana na changamoto ya kutokulipa kodi pindi yanapoenda kuchukua rasilimali hiyo kwenye migodi ya nchi hiyo kuja nchini. 

Ufafanuzi wa madareva hao wanadai kwenye migodi wanakochukua rasilimali hizo wamepata taarifa kuwa wanalipa malipo hayo kwa wamiliki wa magari hayo ‘Risk Allawance’ ambayo  wao kama wasafirishaji walipaswa kuwa sehemu ya mgao ili kupoza machungu ya ugumu wa kusafirisha wakiwa njiani.

Kutokana na changamoto hiyo, Balozi wa Tanzania nchini DRC, Said Mshana amesema amekutana na kuzungumza na Fifi Saini, Gavana wa Jimbo la Lualaba kujadili changamoto zinazowakabili madereva wa malori ya masafa marefu kutoka Tanzania.

“Gavana amenieleza ataitisha kikao baina Serikali ya DRC na wadau mbalimbali wa ndani na nje ya DRC ambacho kesho kinatarajiwa kutoa maazimio ya kutatua changamoto za madereva na wasafirishaji nchini DRC,“ amesema.


Mzizi wa malalamiko

Kelvin Sokoro dereva kutoka Kampuni ya Somikaa amesema mzizi wa mgomo huo umeanza baada ya kubainika mwenzao mmoja alikuwa anaugua na hawakuwa na fedha walipoenda kwenye kiongozi wa mgodi kuomba msaada walijibiwa hawezi kuwasaidia kwa kuwa wao wanalipa malipo ya hatari katika kazi.

“Tuliambia huwa wanalipa kwa kila gari Dola 500 na hawawezi kutusaidia kutupa fedha kumpeleka dereva mwenzetu kwenda hospitali kutibiwa tulishangaa, na si madereva wa Tanzania tu, Zambia, Zimbabwe na mataifa mengine yanayochukua madini migodi ya  DRC,” amesema Sokoro.

Sokoro ambaye kwa sasa yupo Lilonngwe nchini Malawi amesema fedha hiyo ni kweli inatolewa lakini kwakuwa wamiliki wanalijua hilo wanapaswa kutumia utashi kuwapa haki yao licha ya kwamba wao kama madereva hawaiingi mikataba na makampuni hayo.

“Miaka ya nyuma mbona tulikuwa tunapewa ingawa ilikuwa dola 200 na ilikuwa inatolewa ukianza safari lakini baadae walibadilisha utaratibu unapewa ukishafika Dar es Salaam na mzigo na sababu ya kubadilisha madereva wengi walikuwa wanalewa njiani na wanashindwa kufikisha kwa wakati na sasa hivi hawatupi kabisa,”amesema.

Amesema wataendelea kugoma hadi wanachohitaji kipatiwe ufumbuzi

Godlove John ni miongoni mwa madereva waliogoma amesema amechoka kufanya kazi hiyo kwakuwa waajiri wao wanawaona kama takataka kwa kushindwa kuwapatia haki yao kutokana na kazi wanazofanya.

“Tunabebeshwa sumu na madini hakuna malipo wakati taratibu zinataka tulipwe tunabebeshwa tunapata athari nyingi kuumia na wengine kuibiwa mali hizo alafu nakuta wanatupeleka mahakamani na wengine wanafungwa sasa kwanini haki yetu tusiwepewe,”amesema.

Amesema kazi hiyo imeshakuwa ngumu kwa madereva wa Tanzania kwakuwa kila kitu kinachukuliwa na wamiliki wa magari hayo na kuwaacha wao wakiangaika katika mazingira magumu.

“Nyongo iliyoingiwa na madereva nikutaka kurudisha magari hawataki kuendesha kwakuwa wanapita katika mazingira magumu,”amesema

Tatoa.

Mwenyekiti wa Chama cha Malori Tanzania (Tatoa), Chuki Shahaban amesema wanalifuatilia kupata ufumbuzi kwa kushirikiana na ubalozi kwakuwa  Watanzania wanapakia mizigo ya makampuni ambayo yanaubia na migodi mikubwa kule Kongo na hakuna mtanzani mwenye mkataba na migodi hiyo.

Amesema walikuwa na mkutano wa siku tatu kuanzia juzi Tunduma mkoani Songwe kwenye mpaka kati ya Zambia na Tanzania kujadili suala hilo.

“Moja ya mambo tuliyokuwa tunajadili ni hilo kwakuwa hata madereva wa Zambia nao wamegoma na walikuwa wamehamasisha gari hakuna kuingia barabarani kama limebeba madini hayo likijitokeza litapigwa mawe,”amesema.

Pia amesema waliunda kamati iliyoenda Lubumbashi nchini Kongo,kufuatilia kwenye migodi hiyo kujua ukweli kama hayo malipo wanatoa ili wajue namna ya kuwasaidia madereva wapate haki yao.

“Katika uchunguzi wa kamati tumebaini hakuna mgodi unaolipa  posho hiyo  na wao wanashangaa na wanasema wao wanaingia mikataba na mawakala na makampuni na hawajawai kuingia mikataba na madereva kwani hawawajui,”amesema