Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mabaki ya mwili wa aliyepotea yapatikana

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Rukwa wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Muktasari:

  • Mabaki hayo ni ya Sadick Sanga aliyeripotiwa kupotea Machi mwaka huu, watu wawili mbaroni kwa tuhuma za mauaji ya mtu huyo.

Rukwa. Jeshi la Polisi Mkoa wa Rukwa linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kumuua Sadick Sanga (52), kwa kumpiga na kitu kizito kichwani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi (SACP) Shadrack Masija, amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Edward Yohana (3) na Shadrack Bernard (27), wote wakazi wa Kijiji cha Utengule, Wilaya ya Kalambo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Juni 25, 2025, kamanda Masija amesema mabaki hayo ya Sadick yaligunduliwa mchana wa Juni 20 katika Msitu wa Sanganyama, uliopo katika Kijiji cha Utengule, wilayani Kalambo.

Amesema mabaki hayo ni mifupa na fuvu, pia nguo iliyotambuliwa kuwa ni ya Sadick, ambaye aliripotiwa kupotea Machi 2025.

“Mabaki hayo yalitambuliwa na ndugu wa Sadick kwa kutambua nguo zake katika eneo hilo,” amesema Kamanda.

Aidha, ametaja chanzo cha mauaji hayo kuwa ni wivu wa mapenzi, ambapo marehemu alidaiwa kuwa na uhusiano na mke wa mmoja wa watuhumiwa, na hivyo walipanga kulipiza kisasi kwa kumuadhibu.

“Jeshi la Polisi linawataka wananchi waache vitendo vya kujichukulia sheria mkononi, na badala yake watumie njia sahihi zisizoleta madhara kwa jamii,” amesema.

Pia, ametoa wito kwamba taarifa za watu waliopotea zifikishwe polisi, na wananchi watoe ushirikiano wa kutosha kwa Jeshi la Polisi kumtafuta aliyepotea.

Pamoja na hayo, Kamanda Masija ametoa onyo kwa baadhi ya watu wanaosambaza taarifa zisizo na ukweli kuhusu mtu aliyepotea au jambo lolote, watashughulikiwa.

Amesema watuhumiwa hao wako mikononi mwa Jeshi la Polisi, na watafikishwa mahakamani ili hatua stahiki zichukuliwe kwa wote.