Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Saba mbaroni kwa tuhuma za mauaji nyumbani kwa mganga

Wananchi  wa Kijiji Cha Makuro wakiwa katika taharuki iliyotokea ya miili kufukuliwa kwa mganga wa kienyeji mkoani Singida.

Muktasari:

  • Mauaji hayo yanadaiwa kuwa ni kafara baada ya mganga huyo kushirikiana na watuhumiwa kutokana na mgogoro wa ardhi.

Dodoma. Jeshi la Polisi linawashilikilia watu saba kwa tuhuma za mauaji ya watu watatu waliofukuliwa nyumbani kwa mganga wa kienyeji mkoani Singida, Nkamba Kasubi.

Mbali na hilo, miili miwili kati ya mitatu iliyofukuliwa nyumbani kwa mganga huyo, imetambulika kuwa ni ya  Samwaja Said na Gidion Mnyawi (53).

Katika taarifa iliyotolewa leo Jumatatu Agosti 26, 2024 na Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime imewataja watuhumiwa hao kuwa ni Selemani Hango na Said Mangu.

Wengine ni Nkamba Kasubi, Asha Bakari, Awadhi Wawa, Hawa Sumwa na Iddi Hussein Iddi.

Misime amesema baada ya kukamatwa watuhumiwa Hango, Mangu na Kasubi waliongozana na polisi hadi walipokuwa wamemfukia Said baada ya kumuua, kukata sehemu za siri, kisha kuufukia mwili katika shimo.

Amesema kwa msaada na ushirikiano mkubwa wa wananchi Agosti 24, 2024 mashimo mawili yalibainika na baada ya kufukuliwa ulipatikana mwili wa Mnyawi ambaye mara ya mwisho alionekana akiwa amepakizwa kwenye pikipiki ya watu wawili Oktoba 15, 2023.

“Taarifa za kupotea kwake ziliripotiwa polisi na kuwa mwili mwingine ambao haujatambulia  unahitaji mwendelezo wa uchunguzi wa wataalamu wa kuchunguza maiti DNA iliyokuwa ni mabaki ya nyonga, paja  la mguu wa kulia na kushoto,” amesema.

Amesema mabaki ya miili ya watu hao wawili yamebainika baada ya wananchi na askari kuonyeshwa na Asha Migugu ambaye ni mke wa Awadh Wawa ambao ni wakwe wa mganga wa kienyeji aliyekamatwa awali.

Amesema kuwa watu hao waliuawa na mkwe wake huyo akishirikiana na Hango na Salum Awadhi ambaye bado anatafutwa na polisi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Polisi, inadaiwa chanzo cha Mnyawi kuuawa ni kutokana na kitendo cha kuuza shamba mara mbili ambapo aliwauzia wakazi wa Makuro, Hawa Sumwa (54) na Iddi Hussein Idd (25), lakini baadaye ikabainika shamba hilo alishauza tena kwa mtu mwingine.

“Hawa Sumwa na Idd Hussein Idd walifikisha jambo hilo kwa mganga huyo wa kienyeji, naye akamwambia ili fedha zao zirudi inabidi Gidion Samwel atolewe kafara na ndipo mauaji hayao yakapangwa kufanyika,” amesema.