Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lipumba ampa ‘zigo’ la Katiba Mpya Rais Samia

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amemshauri Rais Samia Suluhu Hassan kuanzisha mabadiliko ya Katiba na kuibeba hiyo kama ajenda katika Uchaguzi Mkuu 2025.

Profesa Lipumba ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) amesema kituo hicho kiliona muda uliobaki hautoshi kufanyika kwa mabadiliko ya katiba yote hivyo kuna baadhi ya maeneo yanatakiwa kubadilishwa kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025.

Akizungumza leo wakati wa mkutano maalumu wa baraza la vyama vya siasa na wadau wa demokrasia Profesa Lipumba amesema endapo Rais atafanya marekebisho hayo anaweza kuitumia kama ajenda katika Uchaguzi Mkuu.

Amesema mkutano uliofanywa na kituo hicho kujadili hali ya demokrasia nchini kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025 ulijadili mambo kadhaa ikiwemo suala la katiba.

Kuhusu suala la hilo Profesa Lipumba ameeleza kuwa mkutano ulibaini kuwa muda uliobaki ingekuwa vigumu kukamilisha mchakato wa kupata katiba mpya hivyo mapendekezo ilikuwa kufanyia marekebisho vifungu muhimu.

“Mzee Cheyo alitukumbusha chini ya uongozi wa Kinana akiwa mwenyekiti TCD ilitoa mapendekezo ya kufanya mabadiliko madogo kwenye katiba iliyopo ili tuweze kujenga mazingira mazuri kuelekea chaguzi zijazo,” amesema Profesa Lipumba.

Ameyataja mambo hayo ni tume huru ya uchaguzi na hususani kufanya mabadiliko ya kifungu cha 74 cha katiba iliyopo ili tume huru hiyo iweze kusimamia chaguzi zijazo. Kuwepo kwa mgombea binafsi na matokeo ya uchaguzi wa Rais kuhojiwa mahakamani.

“Tuna imani kwa mapendekezo haya yanaweza kutujengea misingi mizuri ya kuelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025.

“Ikiwa mambo haya utayasimamia inaweza kuwa ajenda nzuri kwako kwamba nahitaji kukamilisha mabadiliko niliyoyaanzisha, ukienda na ajenda hiyo 2025 kutakuwa na kazi kubwa ya kuipiku ajenda hiyo. Tunachosema hapa ni kukutia moyo kwamba haya mabadiliko yaanzishe na ile huruma yako ya kujali hata mtu wa kawaida ukiendelea na hilo utakuwa na ajenda nzuri 2025,” amesema.