Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Latra Mbeya yapiga ‘stop’ kupanda nauli

Muktasari:

  • Latra Mbeya yapiga marufuku upandishwaji nauli kiholela za daladala, ni kufuatia malalamiko ya abiria kuwepo kwa baadhi ya madereva wa daladala kupandisha nauli kutoka Sh 500, 800 hadi 1,000 kulingana na umbali wa vituo.

Mbeya. Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (Latra) Mkoa wa Mbeya, imewapiga ''stop'' wamiliki  na madereva wa vyombo vya usafiri wa umma kupandisha nauli kiholela huku ikitahadharisha watakao bainika kutozwa faini isiyopungua Sh25, 000.

Maamuzi hayo yamefikiwa baada ya kupanda kiholela kwa nauli za daladala katikati ya Jiji la Mbeya hali iliyozua taharuki kwa wananchi wanaotumia usafiri huo.

Ofisa Mfawidhi Latra Mkoa wa Mbeya, Omary Ayoub ameiambia Mwananchi Digital leo Alhamisi Oktoba 12, 2023 kumekuwepo na malalamiko ya wananchi huku sababu kubwa ikitajwa mfumuko wa bei ya mafuta.

“Kuna utaratibu wa Serikali kunapotokea mabadiliko inatangaza sasa kabla ya tamko kutolewa wao wamepandisha nauli, hiyo ni kinyumbe cha sheria za leseni za usafirishaji,” amesema.

Aidha Ayoub amesema kuwa tangu Oktoba 11, 2023 wamepokea taarifa ya mabasi saba ya abiria yamepandisha nauli kinyume cha utaratibu na tayari yamefuatiliwa na kutozwa faini,” amesema.

Ayoub amesema kufuatia hali hiyo tayari kuna oparesheni zimeanza na maofisa wa Latra wako maeneo mbalimbali kufuatilia ili kuwabaini na kuwachukulia hatua za kisheria sambamba na wataokuwa na makosa zaidi kufutiwa leseni za usafirishaji

“Tunatambua kwa sasa mafuta yamepanda kwenye soko la dunia tunaomba wamiliki, madereva kusubiri utaratibu wa Serikali na mwenye mamlaka ya kutangaza ongezeko la nauli ni Waziri mwenye dhamana,” amesema

“Nitoe pole kwa abiria ambao wanakumbana na changamoto hiyo na kuanzia sasa tunaomba ushirikiano...kondakta atakayedai nauli kinyume na utaratibu, wasiliana nasi kupitia namba 0738000063 kwa njia ya wasap au meseji za kawaida,” amesema.

Mfanyabiashara, Elizabeth Joan amesema nauli hizo zimepanda kutoka Sh800 mpaka 1,000 kutoka Uyole mpaka Sokomatola jambo ambalo limechangia kuleta usumbufu.

“Sasa unakuta mtu umebeba nauli ambayo unajua unakwenda na kurudi katika safari yako unapolipa mnaanza mabishano na kondakta kwa madai Serikali imetangaza nauli mpya,” amesema.

Amesema kutokana na hali hiyo wanajikuta wakiwa katika wakati mgumu hususan kwa watu ambao wanakuwa hawana akiba ya pesa kushindwa kumudu gharama hizo.

Kwa upande mwingine, Subira Joel ameomba Serikali kuchukua hatua kwa madereva na makondakta kwani wamekuwa na kauli chafu pindi wanapokuwa wakidai nauli tofauti na iliyozoeleka.

Hata hivyo, Kondakta wa Daladala ya Sokomatola – Uyole, Ezekiel  Daudi amesema wanalazimika kufanya hivyo ili kifikia malengo ya wamiliki wa vyombo hivyo kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta.