Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Latra yapiga ‘stop’ mabasi 38 New Force kusafirisha abiria usiku

Muktasari:

Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (Latra) imesitisha ratiba za mabasi 38 ya Kampuni ya mabasi ya New Force yanayoanza safari kuanzia saa 9:00 na saa 11 alfajiri.

Dar es Salaam. Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (Latra) imesitisha ratiba za mabasi 38 ya Kampuni ya mabasi ya New Force yanayoanza safari kuanzia saa 9:00 na saa 11 alfajiri.

Hatua hiyo imechukuliwa kutokana na hivi karibuni kushuhudiwa ajali za mabasi matano ya abiria ndani ya wiki nne na kusababisha madhara kwa abiria.

Akizungumza Dar es Salaam leo Jumatatu Julai 3, 2023 wakati anatoa uamuzi huo, Mkurugenzi  wa Latra, Habibu Saluo amesema kutokana na wimbi la ajali kwa mabasi ya kampuni hiyo, walifanya uchunguzi na kubaini uvunjaji wa sheria kwa makusudi wa kanuni za usafirishaji wa magari.

"Kampuni ya New Force ni miongoni mwa watoa huduma waliopewa ratiba za saa 9:00 alfajiri mabasi 10 na saa 11:00 alfajiri mabasi 28 na walipewa sharti la kuhakikisha sheria zinazingatiwa lakini kwa makosa haya tunasitisha ratiba yao," amesema.

Amesema kuanzia Julai 5 mwaka huu yatafanya safari zake kuanzia saa 12:00 asubuhi na kuendelea, huku akieleza orodha ya mabasi 38 imeambatanishwa kwenye taarifa waliyopewa na kwamba hatua hiyo siyo adhabu bali ni utaratibu wa kidhibiti ajali unaochukuliwa kwa shabaha ya kuhakikisha usalama wa abiria.

Baada ya kusitishwa kwa ratiba hiyo, Meneja wa Kampuni ya New Force, Masumbuko Masuke amejitetea kuwa kabla ya mamlaka kusitisha ratiba zao walipanga kupunguza magari na kufanya tathimini.

"Hizi ajali zilizotokea kama kampuni zimetupa hasara kubwa na tulikuwa tumepanga kuanzia Jumamosi ijayo tuanze kupunguza mabasi tubakiwe na machache tumudu kuyasimamia," amesema meneja huyo.

Amesema kampuni hiyo inayomilikiwa na raia wa China ina mabasi mengi yanayoenda mikoa mbalimbali na wana madereva 98, wamejipanga kupunguza mabasi ili kuruhusu madereva warudi shule.

Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri (Latracc), Ngowi Leo amesema hatua iliyochukuliwa na Latra ni nzuri na kwamba wao kama washauri wanatamani abiria wanakuwa salama hadi mwisho wa safari zao.