Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kitumbeine wapatiwa vifaa vya upasuaji

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NCBA Tanzania, Claver Serumaga (kushoto) akikabidhi misaada wa vifaa vya upasuaji kwa ajili ya wanawake wanaoshindwa kujifungua kwa njia ya kawaida ikipokelewa na Mganga Mkuu wa Mkoa Dk Silvia Mamkwe (katikati) na kulia ni Mganga Mkuu wa Wilaya ya Longido, Dk Selemani Mtenjela.

Muktasari:

  • Wanawake wa jamii ya Kimaasai wanaoshindwa kujifungua kwa njia ya kawaida sasa kufanyiwa upasuaji katika kituo cha afya Kitumbeine kilichoko wilaya ya Longido mkoani Arusha.

Arusha. Wanawake wa jamii ya Kimaasai wanaoshindwa kujifungua kwa njia ya kawaida sasa kufanyiwa upasuaji katika kituo cha afya Kitumbeine kilichoko wilaya ya Longido mkoani Arusha.

 Hatua hiyo imekuja baada ya kituo cha afya Kitumbeine kupatiwa vifaa vya upasuaji na benki ya NCBA, hali inayokwenda kuwaokoa wanawake hao kutembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo.

Kituo hicho kilichopo kata ya Kitumbeine hadi kukamilika kimegharimu jumla ya milioni 800 zilizotolewa na Serikali.

Akizungumzia msaada huo, Mganga Mmkuu wa Mkoa Dk Silvia Mamkwe alisema kuwa kituo hicho kilichoanza kutoa huduma za afya kwa wagonjwa wa nje na ndani, kilikuwa kikikabiliwa na changamoto ya ukosefu wa vifaa tiba katika masuala ya upasiaji.

"Hali hiyo ilikuwa ngumu sana hivyo wanawake hao kulazimika kupewa rufaa ya kufuata Hospital ya Wilaya ya Longido iliyoko zaidi ya kilomita 60,"

Alisema kuwa wanaishukuru benki ya NCBA kwa msaada huo na sasa wanakwenda kuwasaidia wanawake wenye kuhitaji hudma hiyo maana mwanzoni walihatarisha maisha yao nay a mtoto kwa kufuata huduma hiyo mbali.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NCBA Tanzania, Claver Serumaga, akikabidhi misaada hiyo amesema msaada huo unajumuisha kitanda, vipimo kwa wanawake pamoja na mashine maalum ya kutoa dawa ya usingizi vyenye thamani ya Sh2 milioni.

"Tunataka kuunga mkono juhudi za serikali katika kuhakikisha huduma za matibabu zinapatikana na zenye ubora hivyo kwa mwanzo huu tutaendelea kufuatilia mahitaji zaidi na kujitoa kusaidia hasa jamii za pembezoni," amesema.

Kwa upande wake Dk Frank Kimbwereza Mganga Mfawidhi kituo hicho, alisema kuwa kituo cha Afya Kitumbeine kinahudumia wakazi wote wa vijiji jirani ambao hawana uwezo wa kusafiri hadi Longido mjini kufuata huduma za matibabu.

Hata hivyo, kwa mujibu wa Dk Kimbwereza, kituo hicho kipya cha matibabu bado kinahitaji vifaa vingi ili kiweze kufanya kazi kikamilifu na kutoa shukrani kwa Benki ya NCBA iliyotoa msaada wa kitanda cha kufanyia uchunguzi pamoja na vifaa vya upasuaji.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Longido, Dk Selemani Mtenjela alibainisha kuwa wakaazi wengi wa eneo hilo wanaishi mbali na huduma za afya na kwamba kituo hicho kipo kwaajili a kuhakikisha watu wote katika eneo hilo wanahudumiwa.

Longido inakaliwa na wafugaji wengi wa Wamaasai wanaohamahama ambao asili ya maisha yao ya kifugaji ni kuhama kutoka eneo moja hadi jingine kutafuta malisho na maji kwa mifugo yao.