Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

King’eng’ena awafunda UVCCM kuhusu rushwa

Muktasari:

  • Katibu wa Siasa na Oganaizesheni wa jumuiya ya wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Said King’eng’ena amesema rushwa bado ni mtihani mkubwa katika chama hicho, na kuwataka vijana kusimama kuipinga na kuikataa, ili kuwezesha wale wenye sifa za kuwa viongozi kupata nafasi kwenye chama na serikalini.

Moshi. Katibu wa Siasa na Oganaizesheni wa jumuiya ya wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Said King’eng’ena amesema rushwa bado ni mtihani mkubwa katika chama hicho, na kuwataka vijana kusimama kuipinga na kuikataa, ili kuwezesha wale wenye sifa za kuwa viongozi kupata nafasi kwenye chama na serikalini.

King’eng’ena ameyasema hayo leo Jumapili Julai 16, 2023 wakati akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM) Wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani Kilimanjaro.

Amesema katika kipindi hiki cha kujipanga na uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwakani na uchaguzi mkuu 2025, ni vyema vijana wakakisaidia chama kutokomeza rushwa kwa kutoa taarifa za wale wanaosaka madaraka kwa rushwa.

“Sisi tuna mtihani mkubwa sasa wa rushwa kwenye chama chetu, ninyi vijana mnaweza kuwa mna uwezo mkubwa kwa sababu mmesoma, uwezo wa kutuongoza mnao, lakini hamuwezi kupata dhamana ya uongozi kwenye chama chenu na kwenye serikali kwa sababu hamna uwezo wa kutoa rushwa, hamna fedha za kutoa ili mchaguliwe”

“Sasa kazi yenu ninyi kama vijana kuweni mstari wa mbele kutuambia hapana hatutaki rushwa lakini mkianza kubeba mikoba ya watu ndio mtaanza kuua chama, na ninyi mnaiondoa nafasi yenu ya kuwa viongozi,”ameongeza.


Akizungumza Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Moshi Vijijini, Yuvenal Shirima amesema watakuwa mstari wa mbele kukemea na kipiga vita vitendo vya rushwa katika kipindi cha uchaguzi ili kuhakikisha wote wenye sifa wanapata fursa za kuwa viongozi.

“Viongozi wa vijana Moshi vijijini tutakuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha tunakemea vikali vitendo vya rushwa, tutapita kwenye kata kuzungumza na wananchi na kuwashauri kila mmoja kukataa rushwa katika kipindi cha uchaguzi ili kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais wetu za kutokomeza rushwa,”amesema Shirima.