Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kilio gharama uzalishaji chatawala kongamano la korosho

Muktasari:

  • Kongamano la Kimataifa la Korosho, limeibua hoja mbalimbali zinazoshauri mazingira ya kushawishi vijana wengi kuingia kwenye sekta ya kilimo huku wakulima wakiitaka Serikali kutazama mazingira ya kisera ili kupunguza gharama za uzalishaji.

Dar es Salaam. Kongamano la Kimataifa la Korosho, limeibua hoja mbalimbali zinazoshauri mazingira ya kushawishi vijana wengi kuingia kwenye sekta ya kilimo huku wakulima wakiitaka Serikali kutazama mazingira ya kisera ili kupunguza gharama za uzalishaji.

Baadhi ya wadau hususani wakulima na viongozi wa halmashauri wameshauri Serikali kuweka ruzuku katika mbolea na viuatilifu mbalimbali hatua itakayopunguza mzigo wa gharama za uzalishaji.

Uzoefu unaonyesha mkulima anaweza kunufaika na mche mmoja wa korosho kwa kuvunwa hadi mara mbili kulingana na ubora wa mbegu na mazingira ya hali ya hewa inayotegemea eneo husika. 

Akiuliza swali mbele ya kongamano hilo leo Oktoba 12, 2023, mkulima wa korosho kutoka mkoani Lindi Casmin Mbinga, amehoji mazingira ya wakulima kulazimishwa kuuuza korosho kwa bei ya hasara bila kujali gharama za uzalishaji.

“Kuna wakati Chama chetu cha Ushirika cha Lindi Mwambao kinatangaza mnada wa kuuza korosho, wakulima tunakataa wanaenda kutangaza eneo lingine na kusema wengi wamekubali kuuza, lakini bei ni hasara,”alihoji mkulima jana wakati wa kufunga kongamano hilo la siku mbili.

Akijibu hoja hiyo ya bei mbele ya washiriki, Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), Brigedia Jenerali Alyoce Mwanjile alisema

Kwa mujibu wa ya utafiti wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (Tari) Tawi la Naliendele, unaonyesha mwaka 2020/21, gharama za kuzalisha kilo moja zilikuwa Sh1, 470 katika makadirio ya bei ya soko kati ya Sh1, 700 hadi Sh2, 700 inayobadilika kulingana na mahitaji ya soko.

Kwa mfano, wakulima wa korosho Halmshauri ya Wilaya ya Korogwe kwa msimu wa 2021/22 walilazimika kuuza korosho yao Sh1,487 kwa kilo mnada wa kwanza, Sh1,600 mnada wa pili na Sh1,700 kwa mnada wa tatu ikilinganishwa na gharama hizo za uzalishaji.

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Kallaghe Yusuph alishauri Serikali kutazama gharama za uzalishaji ili kushawishi wakulima wengi. “Ni kweli bei haiaminiki, ni utashi wa wanunuzi lakini Serikali inaweza kuweka ruzuku katika mbolea na dawa, itamsaidia mkulima kupunguza gharama za uzalishaji.”

Hoja hiyo pia iliunga mkono na Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Muheza, mkoani Tanga Erasto Muhina aliyesisitiza umuhimu wa kutazama tozo zilizopo pia. “Kwa anayeanza kuingia kwenye kilimo hiki itakuwa changamoto sana, kwa mfano gharama za dawa ni kubwa sana.”

Pamoja na hoja hiyo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Handeni, Musa Mwanyumba alishauri pia tafiti zinazoandaliwa na TARI zipelekwe kwa wakulima vijijini badala ya kufungiwa kabatini.

“Kwa mfano wanasema kuna tafiti za mbegu, watuambie mbegu ya mche gani inaweza kuhimili mazingira gani ili kuwa na uzalishaji wa tija, hizo ndio taarifa wanataka kusikia wakulima,”alisema Mwayumbu.

Hata hivyo George Listram, mmiliki wa kiwanda cha kubangua korosho ghafi cha Mama cashew, kilichopo mkoani Mtwara alisema changamoto hiyo ya bei inathiriwa na mazingira ya wanunuzi wanaotawala soko la korosho.

“Kuna wanunuzi wawili tu. India na Vietnam, ikitokea msimu fulani Vietnam ana akiba ya kutosha, basi India atakuwa peke yake kwenye soko kwa hiyo anaweza kupanga bei anavyotaka, kwa hiyo bei ni rahisi kushuka na kuathiri wakulima moja kwa moja,”alisema Listram.

Kwa mujibu wa Tari, zaidi ya kaya 700,000 zinajiajiri katika sekta hiyo huku asilimia 95 ya shughuli zote za kujiajiri zikifanywa na wanawake.

“Kuna keki, siagi, juisi, kashata, lakini kwenye mabibo unaweza kuzalisha vinywaji mbalimbali, pia kuna nyama za mabibo watu hawajui,”amesema Brigedia Jenerali Mwanjile kuhusu sekta hiyo iliyochangia asilimia 15 ya fedha za kigeni mwaka jana.

Kwa mujibu wa Tari, asilimia 56 ya waliojiri sekta hiyo ndio wanatumia teknolojia mbalimbali katika eneo la ekari za mikorosho milioni 2.1 katika mikoa husika inayokadiriwa kuwa mikorosho milioni milioni 56.

Kuhusu uzalishaji, umeendelea kukua kutoka tani 0.3 mwaka 1945 hadi tani 236,000 mwaka 2020/21 kupitia matumizi ya mbunge hizo bora, matumizi ya kanuni za kilimo na udhibiti wa magonjwa.