Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kilimanjaro Express kulipa Sh300 milioni kwa ajali iliyoua

Muktasari:

Kampuni ya mabasi ya Kilimanjaro Express imeamuriwa kuilipa fidia ya Sh300 milioni kutoka na kugonga gari dogo na kusababisha mmoja wa wanafamilia waliokuwemo katika gari hilo dogo kupoteza maisha.

Dar es Salaam. Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salam imeiamuru kampuni ya Kilimanjaro Truck Company Limited, inayomiliki mabasi ya Kilimanjaro Express kulipa fidia ya Sh300 milioni kutokana na moja ya mabasi yake kugonga gari dogo lililokuwa linatumiwa na familia na kusababisha kifo cha mmoja wa wanafamilia.

Amri hiyo imetolewa leo Jumatano Desemba 21, 2022 na Jaji Leila Mgonya katika hukumu ya kesi ya madai iliyofunguliwa na mfanyabiashara Leonard Paul Kisena dhidi ya kampuni hiyo, Roland Sawaya (mkurugenzi mtendaji na mmiliki wa kampuni hiyo) na dereva wa basi hilo, Mjahid Mohamed.

Ajali hiyo ilitokea Desemba 24, 2021 eneo la Kerege wilayani Bagamoyo mkoani Pwani, wakati Kisena alipokuwa akisafiri na familia yake kuelekea kwao Kilimanjaro, akitumia gari lake binafsi.

Katika ajali hiyo, basi la Kilimanjaro aina ya Scania lililokuwa likiendeshwa na dereva, Mohamed, kutokea Kilimanjaro kwenda Arusha, liliacha njia na kuliparamia gari la Kisena aina ya Toyota Land Cruiser.

Mtoto wake mmoja wa kike aliyekuwa na umri wa miaka 16 alifariki dunia na Kisena, mkewe na mtoto wao mwingine wa kiume walinisurika japo walipata majeraha.

Dereva huyo alifunguliwa kesi katika Mahakama ya Wilaya ya Bagamoyo akikabiliwa na mashtaka manne, kuendesha gari lisilokuwa na bima, kusababisha kifo, kusababisha majeraha na kusababisha madhara ya uharibifu wa mali kwa kuendesha gari kwa uzembe.

Allikiri makosa hayo na April 5, 2022 na Hakimu Mwanakombo Mmanya alimtia hatiani na kumhuku adhabu ya kulipia faini ya ya jumla ya Sh110,000 kwa makosa yote  au kifungo cha miezi Sita jela akishindwa kulipa faini hiyo.

Baada ya hukumu hiyo ndipo Kisena alipofungua kesi ya madai Mahakama Kuu, akiwakilishwa na wakili Aloys Rugazia.

Katika kesi hiyo ya madai namba 47 ya mwaka 2022, Kisena alikuwa akidai fidia ya Sh400 milioni, ikijumuisha madhara ya jumla na ya hasara halisi kama vile gharama za matengenezo ya gari lake lililoharibiwa, gharama za matibabu ya majeruhi na mazishi ya marehemu.

Jaji Leila Mgonya katika hukumu yake iliyosomwa jana Desemba 20 na Naibu Msajili Joseph Luambano, amekubaliana na hoja za upande wa madai na kuiamuri kampuni hiyo kulipa fidia hiyo na riba ya asilimia Saba kwa mwaka kuanzia tarehe ya hukumu mpaka kukamilisha malipo yote. 

Wakizungumzia hukumu hiyo, Wakili Rugazia Kwa nyakati tofauti walisema kuwa wameridhika na hukumu hiyo kuwa mahakama imetenda haki kwani kwa kiasi fulani imewapa faraja, lakini wakasema kuwa kesi hiyo kwa kiasi kikubwa imefikia huko kutokana na jeuri na kutokujali kwa mmiliki wa kampuni hiyo.

Katika majibu yake dhidi ya madai, kampuni hiyo na mmiliki wake kupitia wakili wake, Michael Ngalo,  walikana kumtambua dereva wa basi hilo kuwa hakuwahi kuwa dereva wa basi hilo, hawamjui na kwamba hawana taarifa za kuwepo kwa ajali hiyo ikilihusisha basi hilo.