Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kiini chatajwa sababu kuibuka maswali ripoti za CAG

Baadhi ya wadau wa Asasi zisizo za kiraia walioshiriki wa mafunzo ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi Mkoa wa Mbeya. Picha na Hawa Mathias

Muktasari:

  • Mafunzo hayo yamelenga kutoa  ukaguzi ya  usambazaji wa toleo maalumu la  Mwananchi la Ripoti za Ukaguzi kwa Asasi za Kiraia (NGO/CSO) katika mikoa mitano nchini.

Mbeya. Ukosefu wa taarifa sahihi za mapato na matumizi ya fedha zinazotolewa na Serikali kutekeleza miradi ya maendeleo ni sababu ya  sintofahamu na kuibuliwa hoja kwenye Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG).

Kufuatia hatua hiyo wadau wa asasi za kiraia wamekuja na mikakati ya kushiriki kufuatilia taarifa za upatikanaji wa fedha utekelezaji miradi ya maendeleo na kujulisha umma.

Hayo yamebainishwa  leo Alhamisi Mei 15,2025 kwenye mafunzo ya ukaguzi wa pamoja na usambazaji wa toleo maalumu la Mwananchi ya Ripoti ya Ukaguzi kwa Asasi za Kiraia (Ngo/Cso), Mkoa wa Mbeya ikiwa ni siku ya pili.

Awali, Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la Saliota Organization kutoka Wilaya ya Mbarali, Elisha Mwanikawaga amesema ukosefu wa taarifa katika ngazi za serikali za mitaa ni changamoto hivyo kama wadau wanapaswa kuisaidia serikali ili kudhibiti ubadhirifu wa fedha umma.

"Tunapaswa sasa kumpunguzia mzigo wa  ufuatiliaji CAG,  kama wadau tushuke huko kufuatilia miradi inayo tekelezwa iendane na thamani ya fedha sambamba na kutoa mrejesho kwa wananchi," amesema.

Amesema mbali na hatua hiyo, wanapaswa kupitia taarifa ya ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali( CAG), kutoa mapendekezo  ili  kuongeza uwajibikaji kwa watendaji wa taasisi za umma nchini.

Awali, akifungua mafunzo hayo jana Mei 14, 2025, Kaimu Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG), Mkoa wa Mbeya, Athuman Seleman amezitaka asazi za kiraia kupitia ripoti iliyowasilishwa na kutoa mapendekezo.

Amesema hatua hiyo italeta chachu ya kuimarisha uwajibikaji na utawala bora wa matumizi ya fedha za umma.

Seleman amesema kwa niaba ya Mkaguzi mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichele na kubainisha mafunzo hayo yameanza jana Mei 14 mpaka Mei 20, 2025 huku mikoa mitano ya Mbeya, Mwanza, Dar es Salaam, Mara na Arusha itanufaika.

"Serikali imeona ni vyema kushirikisha wadau na makundi mbalimbali kuwajengea uelewa wa ripoti ya ukaguzi na kupokea maoni na kuyafanyia kazi, lengo ni kuongeza uwajibikaji katika serikali za mitaa," amesema.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Focus Mauki amesema yapo malengo kadhaa ikiwepo ukaguzi wa hesabu za serikali za mitaa.

"Ili jamii ifikiwe na kupitia taarifa hiyo limeandaliwa Jarida la Mwananchi kwa lugha rahisi ili kuwaweze kuipitia na kutoa maoni na mapendekezo ambayo yatawasilishwa ofisi za  Cag," amesema.

Mkazi wa mabatini, Anitha Solomon amesema changamoto kubwa baadhi ya viongozi wa Serikali za mitaa kutokuwa na utaratibu wa kutoa taarifa za mapato na matumizi ya fedha za miradi kupitia mikutano ya hadhara jambo ambalo linawanyima haki za msingi.

"Hiyo ni mojawapo ya changamoto unakuna miradi inaanzishwa, lakini wananchi hawajui Serikali imetoa kiasi gani ambazo ni kodi zao, ombi letu Serikali itoe maelekezo ya msisitizo ili jamii ijue jinsi matumizi ya kodi zao kuleta maendeleo na siyo kuishia kwenye matumbo ya watu wachache," amesema.