Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kesi ya vigogo NIC kuhamishiwa Mahakama Kuu

Muktasari:

  • Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 365, yakiwemo ya kughushi, kutakatisha fedha na kulisababishia hasara Shirika la Bima la Taifa kiasi cha Sh1.8 bilioni.

Dar es Salaam. Serikali imesema ipo katika hatua za mwisho kuwasilisha nyaraka muhimu Mahakama Kuu ili kesi ya kuchepusha fedha na kuisabishia hasara Shirika la Bima la Taifa (NIC) ya Sh1.8 bilioni, inayowakabili washtakiwa saba akiwemo aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Sam Kamanga, iweze kuendelea na hatua nyingine.

Wakili wa Serikali, Ipyana Mwakatobe, ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo Oktoba 10, 2023, wakati kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 18/2023 ilipoitwa kwa ajili ya kutajwa.

Mbali na Kamanga, washtakiwa wengine ni Tabu Kingu ambaye alikuwa Kaimu Mhasibu Mkuu wa Shirika hilo; Victor Mleleu pamoja na Mhasibu, Peter Nzunda.

Washtakiwa wengine ni Kenan Mpalanguro; Lusubilo Sambo na Mafworo Ngereji.

"Kesi hii imekuja kwa ajili ya kutajwa na upande wa mashtaka tupo katika hatua za mwisho kuwasilisha taarifa muhimu Mahakama Kuu, ili kesi hii iweze kuendelea na hatua nyingine, hivyo kutokana na hali hii tunaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa," amedai Wakili Mwakatobe.

Hakimu Mkazi Mkuu anayesikiliza shauri hilo, Evodia  Kyaruzi, aliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 24, 2023 itakapoatajwa.

Hata hivyo, mshtakiwa Maleleu, Nzunda, Mparanguro na Sambo wanaendelea kubaki rumande kutokana na mashtaka  ya kutakatisha fedha yanayowakabili kutokuwa na  dhamana kwa mujibu wa sheria.

Huku mshtakiwa Kamanga, Kingu na Ngereji wakiwa nje kwa dhamana baada ya kwenda kuomba Mahakama Kuu.

Katika kesi ya msingi, washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka 365, ambayo yapo ya kughushi nyaraka za uongo, kutakatisha fedha, kuwasilisha nyaraka zilizoghushiwa, kichepusha fedha, kuongoza genge la uhalifu na kulisababishia hasara Shirika hilo ya Sh 1.8 bilioni.

Baadhi ya mashtaka yao ni shtaka la kuongoza genge la uhalifu wanalodaiwa kulitenda washtakiwa hao, kati ya Januari Mosi 2013 na Desemba 31, 2018 katika maeneo tofauti tofauti jijini Dar es Salaam mkoani Rukwa, Kilimanjaro,  Arusha, Mbeya, Morogoro na Kigoma, walitenda kosa hilo.

Inadaiwa katika kipindi hicho washtakiwa kwa makusudi waliongoza genge la uhalifu ili kujipatia Sh1.8 bilioni kwa njia ya ulaghai kutoka Shirika la Taifa la Bima.

Katika shatika shtaka la kughushi, linalomkabili Kingu na Nzunda, inadaiwa Mwaka 2013 katika Wilaya ya Ilala, washtakiwa hao wakiwa wahasibu, walighushi hundi yenye thamani ya Sh50 milioni wakionyesha kuwa kuwa ni halali na imetolewa na NIC.

Shtaka la kichepusha fedha, linalowamkabili Kingu, Mleleu, Nzunda na Mpalanguro wanadaiwa Mei 19, 2014 Ilala na Sumbawanga mkoani Rukwa, washtakiwa wanadaiwa kuchepusha kiasi cha Sh50 milioni kutoka katika akaunti inayomilikiwa na NIC iliyopo katika Benki ya NBC kwenda tawi la NIC tawi la Sumbawanga.

Pia mshtakiwa Kingu na Nzunda wanadaiwa kutengeneza hundi ya uongo yenye thamani ya Sh60 milioni wakionyesha ni halisi na imetolewa na NIC, wakati wakijua kuwa ni uongo.